Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
KICHEKESHO: Ajira ngumu!! Cheki hawa walivyoamua kujiajiri
Updated at: 2023-04-29 22:52:42 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Jamaa mmoja alienda kuomba kazi Mbuga ya Wanyama, akaambiwa nafasi ya Kazi ipo ila hakuna Sokwe, "hivyo utajifanya Sokwe na tutakupa ngozi utavaa"
Jamaa siku ya kwanza akavaa, walipokuja watalii mambo yalienda vizuri, Siku iliyofuata Banda lake liliwekwa juu ya Banda la Simba, Jamaa ktk kuongeza mbwembwe akawa anarukaruka, kwa bahati mbaya si akaangukia ndani ya Banda la Simba, akawa anapiga kelele "Mama nakufaaa!"
Mara yule Simba akamwambia "Acha Ufala ww kelele za nini sasa, mimi mwenyewe Binadamu! rudi kwenye Banda lako kabla watalii hawajaja watatushtukia! chezea ajira ww"β¦β¦β¦!!
Updated at: 2024-05-25 17:15:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Pale unapokuwa umefulia sanaβ¦
Mgeni anakutembelea Maskani kwakoβ¦.Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani Mgeniβ¦β¦Unafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite β¦..Bwanaβ¦.Bwana. β¦Bwanaβ¦.Weee ππππππππ
Updated at: 2024-05-25 17:17:50 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mzee moja alikuwa kila usiku anapita mbele ya bank anasimama,kisha anapiga honi,akitoka askari mlinzi,anaondoka.Hilo jambo likamkera sana askari mlinzi, askari akawa na mvizia yule mzee wa kichaga ,siku alipokuja tena akamkamata, akamuuliza kwa nini unakuja unapiga honi kisha unakimbia? Mzee akasema: Haki ya mungu babaangu , Nina pesa zangu ktk account hapa bank naogopa usilale usingizi ndo maana kila siku usiku napita kukuangalia kama umelala!! ππππππ
Hii ndio maana ya Matatizo, usiombee hili likukute
Updated at: 2024-05-25 16:53:58 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Matatizo ni nini???
`Matatizo ni pale unapokuwa umefika ukweni usiku na haja kubwa ikakubana na hukuwa unajua choo kilipo, ukatoka nje na kujisaidia kwenye majani kumbe ni mboga asubuhi ukasikia mama mkwe anasema kuna mjinga kajisaidia kwenye mboga na kaangusha pochi yake hapohapo haa! Vile unajisachi pochi hamna na kulikuwa na passport,vitambulisho, kadi ya benki, pesa zaidi ya laki 2 na nusu, funguo za nyumba yako, ` π€π€π€π€π€π€π€π€π€
Updated at: 2024-05-25 17:59:59 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuna Daktari wa Moyo alifariki wakamchongeaa jeneza lenye umbo la Moyo. Ghafla Daktari mwingine akaanza kucheka, watu wakamuuliza "kwanini unacheka unafurahia mwenzako kufariki?" Daktari yule akajibu "hapana mimi ni Daktari wa kutahiri nafikilia nikifa mtanichongea jeneza lenye umbo la β¦."
Updated at: 2024-05-25 18:09:12 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo! Wakaja unalo babu weee! Ikafuata utajijuuu! Ikafupishwa utajiJJ! Mara ghafla kantangazeee! Haikukaa sana kansajiriii! Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Kweli tamaa ni mbaya, mke wa mtu kaponzwa na tamaa, ndio basi tena
Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake:
JAMAA: Shem nakupenda!
MKE: Hebu toka hapa! Je rafiki
yako akijua? tena koma!
JAMAA: Ntakupa milioni 1!
MKE: Basi njoo kesho mchana
mume wangu akiwa kazini!
Updated at: 2023-04-29 22:53:16 (2 years ago by Melkisedeck Leon Shine)
Jamaa kaenda kwa mke wa rafiki yake: JAMAA: Shem nakupenda! MKE: Hebu toka hapa! Je rafiki yako akijua? tena koma! JAMAA: Ntakupa milioni 1! MKE: Basi njoo kesho mchana mume wangu akiwa kazini!
Kesho yake Jamaa kaja na milioni 1 wakamalizana na mke wa rafki yake, jioni ilipofika Mume akarudi home na kumuuliza Mkewe, "Rafki yangu SAM kaleta hela yangu milioni 1?" MKE akajibu kwa unyonge, "Ndio!" MUME: Yes! Ndio maana nampenda SAM kanikopa asubuhi jioni karejesha!!!! Mke hoiβ¦β¦