Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?
Date: April 17, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki
Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:
β’ Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
β’ Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
β’ Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
β’ Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
β’ Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
β’ Chagua mtu mwenye afya nzuri.
Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.
Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Kuwa na uwazi katika uhusiano wako na msichana ni jambo muhimu kwa sababu inajenga uaminifu na up...
Read More
Ndiyo. Unaweza kufa kutokana na kuvuta sigara au kunywa
pombe. Lakini pale tu utakapozidisha...
Read More
Je, ni lazima kufanya ngono kwa sababu ya marafiki au shinikizo za kisiasa? π€
Ndugu vij...
Read More
Leo tutazungumzia juu ya jinsi ya kuonyesha mapenzi kwa msichana wako. Ingawa kuna njia nyingi to...
Read More
Neno Albino linamaanisha
mtu mweupe, linatokana na
neno la lugha ya Kilatini -
albus-linamaanisha β...
Read More
Mboni katika macho ya Albino haina pigimenti ya rangi. Kwa
hiyo, ni rahisi macho yao kuathir...
Read More
Katika miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua, mwanamke anayenyonyesha mtoto anapata kinga ya m...
Read More
Hapana, ukila na mtu mwenyemaambukizi ya Virusi vya UKIMWI huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI w...
Read More
Njia za Kujenga Mazingira ya Kuaminika katika Uhusiano wako na Msichana
Kamwe hufai kuhisi...
Read More
Ngozi ya Albino ina ukosefu wa rangi. Inaonekana kama ya watu
weupe ambao wana kiasi cha pig...
Read More
Kama unatafuta njia za kufurahisha msichana na shughuli za kujenga timu, basi umefika mahali pazu...
Read More
Je, umewahi kufanya mapenzi ukatumia vifaa vya burudani kama vile vyombo vya muziki au nuru ya ra...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!