Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE 🔁
AckyShine

Chanzo, dalili, aina na matibabu ya ugonjwa wa kifafa

Featured Image
Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme[impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara. Ifahamike kuwa, aina ya kifafa inayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae. Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika. Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu…

Chanzo cha ugonjwa wa kifafa ni nini?

Chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ya hiz ni moja ya sababu za kuugua kifafa. Kurithi; familia na koo zingine zinakua na ugonjwa huu hivyo watoto na wajukuu huzaliwa tayari na ugonjwa huu. Kuumia kichwa: ajali zinazohusisha kuumia kwa kichwa huweza kusababisha kuumia kwa mishipa ya fahamu na mtu kuugua kifafa. Magonjwa mengine; kuna magonjwa mtu akiugua maishani mwake baadae huweza kupata kifafa kwasababu magonjwa hayo yanavyoharibu mfumo wa ubongo.. mfano homa ya uti wa mgongo kitaalamu kama meningitis. Uvimbe kwenye ubongo: matatizo ya uvimbe kwenye ubongo kama kansa huweza kusababisha mtu kuugua kifafa. Kiharusi; huu ni ugonjwa ambao husababishwa na damu kushindwa kupita vizuri kwenye ubongo au kupasuka kwa mishipa ya damu ya ubongo hali hii husababisha mtu kupooza nusu ya mwili wake na huweza kuugua kifafa baadae. Matatizo wakati wa kuzaliwa: wakati mwingine mtoto huzaliwa kwa shida sana kwa njia ya kawaida kiasi kwamba kichwa chake hubanwa sana wakati wa kupita na hali hii huweza kumsababishia kifafa kwanzia utotoni. Matatizo ya utengenezaji wa mtoto tumboni; wakati mwingine ile miezi mitatu ya kwanza ambayo mtoto ndio anapata viungo tumboni huweza kutokea kasoro kwenye mfumo wa fahamu za kwenye ubongo na kumfanya apate kifafa akizaliwa. Magonjwa ya uzee yanayoathiri ubongo; kuna magonjwa huharibu ubongo wakati wa uzee na magonjwa haya huweza kusababisha kifafa kipindi hicho.

Aina za kifafa

Kuna aina mbili kubwa za kifafa:

1)Primary marygeneralized seizures

Hii ndio aina ya kifafa ambayo inafahamika sana mitaani; na inahusisha mgonjwa kukamaa, na kupoteza fahamu, pamoja na dalili zingine kama vile kutoa povu mdomoni, na kujisaidia haja kubwa na/au ndogo bila kujitambua akishikwa na hali hiyo. Pia wengine hupatwa kama na wazimu au kuchanganyikiwa kwa muda kabla au baada ya kushikwa na hali hiyo.

2)Partial seizures

Aina hii ya kifafa ni ile ambayo haihusishi muhusika kupoteza fahamu na kukakamaa!! Bali hushikwa na hali fulani kama ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa; Wengine huwa na dalili zisizoeleweka za mara kwa mara kama vile kusihiwa nguvu, kizungu zungu, kichwa kuuma sana (bila sababu ya kiafya inayojulikana), na kadhalika. Aina hizi za kifafa ziko nyingi, na dalili hutofautiana kwa kadri ya aina ya kifafa!!

Vipimo vinavyofanyika kugundua kifafa

Ugonjwa huu unaweza kutambulika kwa daktari kuchukua historia ya dalili zinazomkabili muhusika tu(hakuna kipimo ambacho kinaweza kutambua kifafa kwa asilimia 100); Kuna kipimo kinachopima jinsi ubongo unavyotoa taarifa za umeme (ELECTROENCEPHALOGRAM-EEG), ambacho kinaweza kutambua kifafa, lakini kipimo hiki kinaweza kikaonekana kuwa hakina shida, na bado mtu akawa na tatizo hilo la kifafa. Hivyo basi, kifafa ni moja kati ya magonjwa machache ambayo kutambulika kwake kunategemea sana ujuzi na utaalamu wa daktari katika kuunganisha dalili za mgonjwa kuliko vipimo!! Hata hivyo, mara nyingi nyingi mgonjwa hupimwa vipimo tofauti ili kuweza kujua chanzo cha ugonjwa… mfano • Uwezo wa kufanya kazi figo • Uwezo wa kufanya kazi maini • Kupima maji ya uti wa mgongo • Kupima Kaswende • Picha ya ubongo mfano CT SCAN. Mambo yanayofanya kupata degedege za kifafa mara kwa mara.. • Kukosa usingizi kwa muda mrefu • Mianga na miale ya disko • Unywaji wa pombe • Kuishiwa sukari mwilini wakati wa akisikia njaa kali. • Kutomeza dawa kama ilivyoelekezwa

Huduma

Matibabu yasiyo ya dawa wakati mgonjwa amekamatwa na kifafa:{non pharmacological treatment}yaani HUDUMA YA KWANZA • Mzuie mgonjwa asijiumize kwa kuweka kitu laini chini ya kichwa chake, ondoa vitu vikali karibu yake kama kisu, sindano au vyuma. • Usilazimishe kitu chochote kwenye mdomo wa mgonjwa. • Usimshike kuzuia mizunguko yake • Weka kichwa alale anaangalia upande mmoja ili kutoa mate mdomoni. • Kaa na mgonjwa mpaka degedege ziishe • Usiweke chochote mdomoni kwa mgonjwa kama dawa au chakula mpaka apate fahamu zake. Mtu mwenye kifafa hali hii ya kukamatwa na degedege za kifafa sio ya ajabu sana ila ukiona dalili hizi mkimbize hospitali.. • Degedege za kifafa zaidi ya dakika kumi • Kutapika sana • Kushindwa kuona vizuri • Kupoteza fahamu • Kichwa kuuma sana.

MATIBABU YA UGONJWA

Kama kawaida chanzo cha ugonjwa kikipatikana mgonjwa huanzishiwa matibabu lakini kama mgonjwa alikua tayari ameshapata madhara kwenye ubongo kulingana na chanzo husika ataendelea kua na kifafa. Ugonjwa wa kifafa hauponi kabisa kwa 100% hospitali, ukishaambiwa una kifafa au mgonjwa wako ana kifafa basi utapewa utaratibu wa matibabu yaani kumeza dawa siku zote za maisha yako na kufuata baadhi ya masharti na utaishi maisha ya kawaida kabisa.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Hatua za kufuata

1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti

2. ... Read More

Madhara ya kunywa soda

Madhara ya kunywa soda

Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dum... Read More

Jinsi ya kufanya kupunguza unene wa mwili kwa haraka

Jinsi ya kufanya kupunguza unene wa mwili kwa haraka

Nichukue wasaa huu kukuarika rasmi ewe mpenzi na mfuatiliaji wa blog hii ya Muungwana blog, naomba n... Read More
Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum , ambaye pia huitwa spirochetes kutokan... Read More
Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia barafu

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia barafu

Barafu inaweza kuzipunguza chunusi zionekane ni ndogo na kupunguza madhara yatokanayo na chunusi.... Read More

Sababu na tiba ya tatizo la kukoroma usiku: Kukoroma unapolala

Sababu na tiba ya tatizo la kukoroma usiku: Kukoroma unapolala

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila ... Read More
Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu

Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu

Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo ... Read More

Vyakula vinavyoongoza kuongeza akili kwenye ubongo

Vyakula vinavyoongoza kuongeza akili kwenye ubongo

BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaout... Read More

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu uotaji wa meno kwa mtoto

Mambo ya msingi kufahamu kuhusu uotaji wa meno kwa mtoto

Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humw... Read More

Vitu ambavyo mama mjamzito hapaswi kutumia

Vitu ambavyo mama mjamzito hapaswi kutumia

Vipo vitu mbalimbali ambavyo mama mjamzito hapaswi kuvitumia wakati wa ujauzito kwani vina athari... Read More

Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

Sababu za Magonjwa ya Figo na jinsi ya kujikinga

JINSI YA KUONDOKANA NA JANGA HATARI LA UGONJWA WA FIGO:*
*1.Usichelewe kwenda HAJA.* Kutunza... Read More

Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Njia za kutibu chunusi bila kwenda hospitali

Chunusi ni nini?