Log in to access your menu with tools for managing ๐ tasks, ๐ฅ clients, ๐ฐ finances, ๐ learning, ๐ personal growth, and ๐ spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:35:22 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa. Hivi leo watu wanatumia vyombo mbalimbali vya usafiri kwenda karibu kila eneo.
Kwa hakika kutembea kwa miguu kuna manufaa mengi sana kwa ajili ya afya ya mwili, uchumi na maisha yako ya kijamii.
Ikiwa unapenda kuwa bora na mwenye tija zaidi katika nyanja zote, basi fahamu faida za kutembea kwa miguu.
Hukabili maradhi ya moyo kwa kuhamasisha mzunguko mzuri wa damu.
Huimarisha mifupa.
Huondoa au kupunguza hatari ya kupata kiharusi.
Husaidia kupunguza uzito.
Huzuia saratani ya utumbo mpana.
Hukuwezesha kupata vitamini D kutoka kwenye jua.
Hukusaidia kuboresha usawa wa mwili wako (balance).
Hukabili maradhi ya kisukari. Unapotembea unafanya mazoezi yanayoleta uwiano wa urefu na uzito โ BMI; jambo litakalokukinga na aina ya pili ya kisukari (Type 2 Diabets).
Hukabili shinikizo la damu.
Huondoa msongo wa mawazo.
Huongeza utayari.
Hukufanya ujifunze mambo mbalimbali kwa kuona.
Hukuokolea gharama za nauli au mafuta.
Hupunguza lehemu mbaya mwilini (cholesterol)
Huimarisha misuli.
Husaidia mmengโenyo wa chakula kwenda vizuri.
Huwezesha kinga mwili kujiimarisha na kujijenga (kutokana na sababu kuwa kutembea ni aina ya zoezi).
Huboresha uwezo wa kumbukumbu.
Hukujengea mahusiano ya kijamii. Unapotembea utakutana na watu mbalimbali.
Huzuia kuzeeka. Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa watu wanaotembea umbali mrefu huishi zaidi.
Hukuweka katika hali nzuri (mood).
Hukusaidia kulala vizuri. Kumbuka mazoezi ni chanzo cha usingizi mzuri.
Huboresha afya ya uzazi hasa kwa wanaume. Kutembea kama zoezi ni njia ya kuwapa wanaume nguvu katika afya ya uzazi.
Huzuia kuharibika kwa mimba. Mazoezi ni muhimu sana kwa mama mjamzito kwa ajili ya afya yake na mtoto; hivyo zoezi rahisi na jepesi kwake ni kutembea.
Huboresha mwonekano wa mwili. Mazoezi ni njia moja wapo ya kuufanya mwili wako uonekane katika umbo zuri. Hivyo kutembea kama aina mojawapo ya zoezi kunaweza kukusaidia sana.
Naamini umeona jinsi ambavyo kutembea kwa miguu kuna manufaa makubwa sana kwenye afya, uchumi na hata mahusiano yako ya kijamii.
Inashauriwa kuhakikisha unatembea kwa miguu angalau dakika 30 kila siku. Kwa njia hii utapata manufaa mengi yaliyotajwa hapo juu.
Namna ya kuongeza nguvu za kiume bila kutumia dawa
Updated at: 2024-05-25 10:35:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa wanaume wengi. Tatizo hili limewakumba wanaume wengi walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta utatuzi kwani tatizo hili huwafanya kuwa na wasiwasi wa maisha. Ndoa nyingi zimevunjika na mahusiano kuharibika kwa sababu ya tatizo hili.
Kwa wanaume wenye umri mkubwa, upungufu wa nguvu za kiume unaweza usiwe ni tatizo kwani miili yao inakuwa tayari imechoka.
Hizi hapa ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kurudisha nguvu za kiume zilizokuwa zimepotea, au kuimarisha uwezo wako wa tendo la ndoa.
Epuka unywaji wa Pombe.
Tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini inakunyima uwezo wa kufanya tendo hilo, kwani hupunguza kiwango cha maji mwilini.
Fanya mazoezi ya viungo.
Watu wengi wameelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupatishi damu ya kutosha kwenda sehemu mbali mbali kama vile ubongo, ini na figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake. Uume ili usimame kwa uimara, unatakiwa upate damu ya kutosha.
Kufanya mazoezi hupunguza kiwango cha mafuta katika mishipa ya damu na kuiwezesha kupeleka damu ya kutosha katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo uume.
Jitahidi kutumia vinywaji na vyakula visivyokuwa na sukari nyingi.
Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi kwani ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. Kula vyakula asili na nafaka ambayo haijakobolewa, kula matunda kwa wingi pamoja na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utakuwa imara katika tendo la ndoa.
Epukana na msongo wa mawazo.
Ufanyaji wa tendo la ndoa huwa unahusisha mambo mengi. Unaweza ukawa umekamilika kiafya lakini ukashindwa kufanya mapenzi kwa kuwa una msongo wa mawazo. Hakikisha kabla ya kwenda faragha na mpenzi wako, unauituliza akili na usiwaze mambo mengine nje ya tendo linaloenda kufanyika. Hii itakupa muda mzuri wa ubongo wako kupeleka damu ya kutosha katika uume.
Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki, chuma, selenium, manganese na vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki. Madni haya huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako. Madini haya hupatikana katika mboga, samaki na matunda ya aina mbalimbali.
Kunywa maji ya kutosha kila siku.
Kunywa maji ya kutosha kila siku, usingoje mpaka kiu ikupate. Mtu mzima anapaswa kunywa maji glass 8 mpaka 10 kwa siku. Maji husaidia kuongeza kiwango cha damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini.
Sababu, dalili na jinsi ya kujikinga na tatizo la kiungulia kwa wanawake wajawazito
Updated at: 2024-05-25 10:35:01 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hii ni hali inayowakumba mama wajawazito walio wengi. Inaweza kutokea kipindi chochote cha ujauzito ila mara nyingi hutokea katika umri wa mimba kuanzia miezi mitatu.
Kiungulia ni nini?
Kiungulia ni maumivu mithili ya moto yanayotokea kifuani sehemu ya katikat ya kifua. Maumivu haya hayana uhusiano na moyo.Yanatokea pale asidi ya kwenye tumbo inapopanda na kurudi kwenye koo la chakula.
Asidi hii ikiwa tumboni haisababishi madhara wala maumivu kwani inazalishwa muda wote na kuta za tumbo kumeng'enya chakula. Seli za kuta za tumbo haziathiriki na asidi hii ndio maana inapokuwa tumboni haileti shida yoyote. Ila seli za kuta za koo la chakula haziwez kustahimili asidi hii ndiyo maana inapopanda kwenye koo la chakula unapata maumivu ya kiungulia.
Dalili ya kiungulia
Kiungulia mara nyingi hutokea wakati unakula au baada ya kula na kinaweza kuzidi makali wakati umelala.
Dalili ni kama, Kuhisi maumivu kama ya kuungua kwenye kifua au chembe moyopamoja na kujisikia radha ya uchachu mdomoni.
Saabu za kiungulia kwa wajawazito.
Sehemu mbali mbali za mwili hupata mabadiliko wakati wa ujauzito. Wakati wa ujauzito mwili hutengeneza kwa wingi hormone ya progesterone na relaxin ambazo huathiri mfumo wa chakula.
Progesterone hormone hii hufanya chakula kutembea na kufyonzwa kwa taratibu sana. Relaxin hormone hufanya misuli laini ya mwili kulegea ikiwemo misuli inayobana sehemu ya juu ya tumbo (sphincter) inayozuia chakula au vitu vya tumboni visirudi kwenye koo la chakula . Mabadiliko haya hufanya kuwa rahisi asidi na chakula vilivyomo tumboni kurudi kwenye koo la chakula na kusababisha kiungulia.
Vitu vingine vinavyoweza kusababisha kiungulia kwa mama mjauzito ni;
Kula chakula kingi sana
Vyakula vyenye viungo
Vyakula vyenye mafuta mengi
Matunda jamii ya limao na machungwa
Chocolate
Soda
Kahawa
Sigara
Pombe
Baadhi ya madawa
Stress
Uzito uliopitiliza.
Jinsi ya kujikinga na kiungulia kwa wajawazito.
Kuwa na uzito unaowiana na urefu wako
Epuka vyakula vinavyosababisha kiungulia kama nilivyoainisha hapo juu
Epuka kula chakula kingi kwa wakati mmoja. Bali kula chakula kidogo kila baada ya muda.
Kunywa maji ya kutosha. Angalau lita moja na zaidi kwa siku
Epuka kuvaa nguo zinazobana sana tumbo na kiuno
Usilale muda mfupi baada ya kula.
Epuka kuwa na msongo wa mawazo /stress
Onana na Daktari kupata ushauri wa dawa za kupunguza makali ya asidi hii ambazo ni salama kwa wajawazito
Updated at: 2024-05-25 10:37:33 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.
Chemsha maji kwenye sufuria jikoni funika na uache nafasi kidgo ya mvuke uwe unatoka, kisha chukua taulo na ujifunike usoni huku ukisogelea karibu na mvuke unapokea na uruhusu mvuke huo ukupate kwa mbali.
Baki hapo kwa dakika 5 mpaka 10 hivi huku ukiwa umetulia (relaxed). Huu mvuke utakusaidia pia kujisikia mtulivu na kukuondolea mfadhaiko wa akili.
Mwishoni mwa zoezi jisafishe uso wako na maji ya baridi.
Endelea kusoma makala hii kujifunza zaidi dawa nyingine za asili za kutibu chunusi.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya Dengu (Dengue fever)
Updated at: 2024-05-25 10:35:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Ugonjwa wa dengue ni tishio la ugonjwa hatari linaongezeka siku hadi siku. Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu aitwae aedes.
Ugonjwa huu huenea zaidi msimu wa nvua. Huchukua siku 3-14 kwa mgonjwa kuonyesha dalili za dengue. Dalili kuu za dengue huwa ni maumivu makali ya kichwa, mgongo pia kutokwa na damu maeneo ya wazi kama puani maskioni (Hasa watoto) .
Siku zote kinga ni bora kuliko tiba hivyo huna budi kufanya yafuatayo kujikinga na ugonjwa hatari wa dengue:
1. Epuka Kuvaa nguo fupi kama kaptura, shati au tisheti kata mikono. Vaa suruali na shati/sweta la mikono mirefu 2. Usiweke Makopo chini ya Viyoyozi kwani hudondosha maji yanayoweza kuwavutia mbu. 3. Maji ya kwenye makopo ya maua yabadilishwe mara kwa mara. 4. Epuka Kuanika nguo Mbichi ndani ya nyumba. Hii huwavuta mbu kuzaliana 5. Osha vyombo visivyotumika angalau mara moja kwa wiki. 6. ondoa madimbwi yoyote yanayotuwamisha maji. 7. Tumia chandarua unapolala nyakati za mchana. 8. Funika makopo ya taka ili kutowavutia mbu. 9. Kunywa maji mengi na jenga mazoea ya kunywa juice za matunda. 10. Usiache milango wala madirisha wazi bila sababu ya msingi.
Updated at: 2024-05-25 10:35:24 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kila wakati unashauriwa na watalam wa afya ya kwamba unatakiwa kula tende kwa wingi ili kupata faida zifuatazo katika mwili wako:
1. Huongeza nguvu kutokana na kuwa na sukari ya asili, unaweza kuchanganya na maziwa na kupata mchanganyiko bora!
2. Huzuia meno kuoza, na ni tiba nzuri kwa wagonjwa wa anemia kutokana na kuwa na madini mengi ya chuma.
3. Hupunguza uwezekano wa kupata Kiharusi (stroke) kwani hazina cholesterol kabisa! Pia zina vitamini na madini kwa wingi.
4. Huongeza uwezo wa Kujamiiana kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nguvu
5. Hupunguza madhara ya pombe mwilini na kurudisha afya ya mtu.
6. Zina kiasi kikubwa cha kamba kamba ambazo hufanya mtu apate choo kirahisi na laini.
7. Licha ya kuwa tamu, tende haziongezi kiwango cha sukari mwilini, hivyo zinaweza kutumika kama mbadala wa sukari
8. Huimarisha Mifupa na kuondoa maumivu ya mara kwa mara ya mifupa kutokana na kuwa na madini ya chuma na potassium kwa wingi.
9. Tende ina msaada mkubwa kwa mama mjamzito, humuongeza nguvu, na hazina madhara kiafya kwa mtoto. Pia husaidia kupata uzazi salama
10. Ulaji wa tende kwa wingi husaidia kuongeza mwili kwa wale waliokonda kupita kiasi. Hivyo hushauriwi kula tende kupita kiasi kama huhitaji kuongeza mwili.
Updated at: 2024-05-25 10:35:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao yamekuwa na rangi, hivyo kuwafanya watu hao kuona aiabu. Pia watu wengi wakiona meno yana rangi ya njano hudhani ni machafu, meusi yanahitaji kusafishwa ili yawe meupe.
Meno kubadilika rangi huweza kuwa ni sababu moja au muunganiko wa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;
Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye kaboni, sigara na mvinyo (wine) kwa muda mrefu husababisha kubadilika kwa rangi ya meno kwa juu (extrinsic staining).
Utumiaji wa maji yenye madini mengi ya fluoride katika kipindi cha utoto (dental fluorosis).
Matumizi ya dawa aina ya tetracycline kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayapata madini ya kutosha.
Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ya juu ya jino (amelogenesis imperfecta). Iwapo sehemu hii imeumbwa ikiwa laini kuliko inavyotakiwa huwa rahisi kufyonza rangi na jino huota likiwa limebadilika rangi au hubadilika baada ya muda.
Kufa kwa sehemu hai ya jino hasa kutokana na kuumia kwa jino au ajali (pulp necrosis), hali hii huweza huchukua miaka mingi mpaka kutokea kubalika rangi ya jino..
Jino liliozibwa kwa kutumia material aina ya amalgam huweza kubadilika rangi na kuwa nyeusi.
Mara nyingne jino lililotibiwa kwenye mzizi wa jino (root canal treatment ) huweza kubadilika rangi baada ya miaka mingi.
Kuna njia mbalimbali ambazo hutumika kuyafanya meno yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kuwa meupe.
Njia hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na jinsi alivyoathirika. Kuna njia nyingi ambazo huweza kuyangโarisha kwa ndani (internal bleaching) au kuyangarisha kwa nje (external bleaching).
Endapo una tatizo la meno yaliyobadilika rangi, muone daktari wa kinywa na meno kwaajili ya ushauri na matibabu kwani kinywa kizuri na chenye afya huongeza kujiamini.
Njia za kutibu shinikizo la chini la damu au presha ya kushuka
Updated at: 2024-05-25 10:35:31 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
๐Kutibu shinikizo la chini la damu kwa kutumia maji chumvi
Kunywa Maji yenye chumvi husaidia kutibu shinikizo la chini la damu sababu sodiamu iliyomo kwenye chumvi hupandisha juu shinikizo la damu. Usizidishe dawa hii kwa sababu chumvi nyingi kuzidi ina madhara kiafya.
Matumizi:
Changanya nusu kijiko cha chai cha chumvi ndani ya maji glasi moja (robo lita) na unywe mchanganyiko huu mara 1 au 2 kwa siku
๐Matumizi ya kahawa kutibu presha ya kushuka au shinikizo la chini la damu
Kahawa husaidia kuongeza presha au shinikizo la damu. Unashauriwa Kunywa kikombe kimoja cha kahawa kunaweza pia kusaidia kupandisha shinikizo lako la damu kwa muda.
Kama unapatwa na kushuka kwa shinikizo la damu mara kwa mara basi kunywa kikombe cha kahawa asubuhi au unywe wakati unakula cha mchana na cha jioni.
Usizidishe matumizi ya kahawa kwakuwa kahawa ina madhara mabaya kwa afya ya mwili kwa ujumla.
๐Matumizi ya zabibu kavu kutibu shinikizo la chini la damu
Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo
1. Chukua zabibu kavu Loweka zabibu 30 mpaka 40 ndani ya kikombe cha maji kwa usiku mzima.
2. Asubuhi kabla ya kula wala kunywa chochote kula zabibu moja baada ya nyingine na unywe pia maji yake
3. Rudia zoezi hili kila siku kwa majuma kadhaa hata mwezi.
๐Matumizi ya Tangawizi kutibu shinikizo la chini la damu
Hatua za kufuata
Chukua Kijiko kikubwa kikubwa cha tangawizi mbichi iliyoparuzwa
Changanya na Kikombe kimoja cha maji ya moto
Chemsha katika moto kwa dakika 12 hivi
Kisha ipua na uchuje
Ikipoa kidogo kunywa yote,
fanya hivi mara 2 kwa siku kila siku
๐Matumizi ya Mrehani (basil) kutibu presha ya kushuka
Hii ni dawa nzuri ya kutibu shinikizo la chini la damu sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C, magnesiamu na potasiamu, vilevile dawa hii husaidia kuweka sawa akili na kuondoa msongo wa mawazo (stress).
Matumizi
Chukua majani 10 mpaka 15 ya mrehani mbichi
Saga au twanga kupata maji maji yake (juisi).
Weka asali kijiko kidogo kimoja ndani yake.
Kunywa mchanganyiko huu kila siku asubuhi ukiamka tu tumbo likiwa tupu.
Vile vile unaweza kutafuna tu moja kwa moja majani kadhaa ya mrehani kila siku asubuhi.
๐Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka
Hatua za kufuata
1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti
2. Weka vijiko vikubwa viwili vya asali ndani yake na kisha changanya vizuri
3. Kunywa yote asubuhi tumbo likiwa tupu na jioni glasi nyingine kwa majuma kadhaa
๐Matumizi ya maji kutibu shinikizo la chini la damu
Matumizi ya maji ya kunywa ni moja ya dawa rahisi kabisa ya shinikizo la chini la damu.
Hii ni kwa sababu Maji ni mhimu kwa kila ogani ndani ya mwili iweze kufanya kazi zake sawa.
Kwa hiyo sababu kuu ya mtu kuwa na shinikizo la chini au hata la juu ni matokeo ya mishipa ya damu kutokuwa na vimiminika vya kutosha.
Mishipa ya damu imeundwa kwa maji maji ya damu (serum) na seli za damu.
Maji yanapopungua kwenye mwili hata vipenyo vya mishipa yako navyo hupungua ukubwa wake jambo linaloleta kushuka kwa shinikizo la damu.
Matatizo yote haya ni matokeo ya kutokunywa maji ya kutosha kila siku.
Kwa sababu hii, ili kupandisha juu shinikizo la damu unahitaji kunywa zaidi maji sambamba na juisi nyingine za matunda au za mboga mboga kila siku.
Hii inasaidia kuongeza vimiminika katika mishipa ya damu.
๐Matumizi ya juisi ya limao kutibu shinikizo la chini la damu
Juisi hii ni nzuri sana katika kutibu shinikizo la juu la damu.
Lakini inaweza pia kutumika kutibu shinikizo la chini la damu hasa ikiwa hili shinikizo la chini la damu limesababishwa na upungufu wa maji mwilini (dehydration).
Kutibu shinikizo la chini la damu unaweza kuchanganya juisi ya limau na chumvi kidogo na sukari au unaweza kutumia maji maji ya miwa.
๐Ulaji mzuri hupunguza uwezekano wa kupata shinikizo la chini la damu
Ni mhimu kula mlo kamili kila siku. Kula lishe duni kunaweza kupelekea kuzalishwa kwa damu isiyo na afya inayoleta shinikizo la damu.
Kula zaidi vyakula vyenye protini, vyenye vitamini B na C kwa wingi. Kula milo midogo midogo hata mitano kuliko kula miwili au mitatu lakini ya nguvu sana.
Unaweza kutumia kitunguu swaumu hasa kibichi ukitafuna punje 2 kila unapoenda kulala kadharika glasi moja ya juisi ya ubuyu kutwa mara 1.
Acha vilevi vyovyote mara tu unapogundulika na shinikizo la chini la damu. Epuka pia vyakula vyenye wanga sana kama tambi, mikate, viazi, wali nk
Upungufu wa baadhi ya vitamini hasa vitamini za kundi B na madini kunaweza pia kuleta shinikizo la chini la damu. Hivyo ili kudhibiti shinikizo la chini la damu unahitaji kula mlo sahihi kila siku.
๐Matumizi ya Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu
Unaweza kutumia Lozi na maziwa kutibu shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo;
Loweka lozi 5 mpaka 6 kwenye kikombe cha maji kwa usiku mmoja
Asubuhi menya hizo lozi na uzisage
Chukua hizo lozi ulizosaga na uweke ndani ya kikombe cha maziwa