Jinsi ya kufanya kupunguza unene wa mwili kwa haraka
Date: April 15, 2022
Author: SW - Melkisedeck Shine
Nichukue wasaa huu kukuarika rasmi ewe mpenzi na mfuatiliaji wa blog hii ya Muungwana blog, naomba nichukue walau dakika zako chache niweze kukueleza kinagaubaga ni kwa jinsi gani unaweza kupunguza mwili wako kwa kutumia hatua zifuatavyo:
1. Zingatia muda wa kula.
Watalamu wa masuala ya afya wanasema muda mzuri wa kula chakula ni masaa manne baada ya kuamka, pia chakula cha mchana kiliwe tena baada ya masaa nne mara baada ya kupata kifungua kinywa, na masaa takribani matatu kabla ya kulala, kufanya hivi huupa mwili wako mda wa kukimenโgenya chakula vizuri na kuyeyusha mafuta yaliyopo kwenye chakula pia. Hivyo unakumbuswa kufanya hivi kila wakati kama kweli unataka kupunguza mwili wako.
2. Epukana msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo au stress hupelekea kula vyakula ambavyo sio sahihi kwa afya yako na kwa wingi kama vile pombe, snacks mfano crips, biskuti, pipi,c hocolate na kadhalika hata hivyo mwili huhifadhi mafuta kwa wingi kipindi ukiwa na stress, hivyo kila wakati epuka kula vyakula ambavyo vitakusababishaia kuwa mwili wenye mafuta.
3. Kutoruka mlo wa asubuhi(breakfast)
Wengi wetu tumejikuta tukimaintain kwa kuruka breakfast na baadae kujikuta tukifidia ule mlo kwa kula chakula kingi zaidi, Kufanya hivi sio kujipunguza bali kukufanya uzidi kunenepa zaidi, hivyo unatakiwa kuzingatia ya kwamba hauli chakula kingi kama mchana hukupata kifungua kinywa, unachotakiwa kufanya ni kula chakula cha kawaida tu.
4. Angalia aina ya chakula.
Aina ya vyakula sahihi tunavyopaswa kula ni vyakula vyenye protein kwa wingi kama vile mboga za majani na matunda kwa wingi pia ,wanga kidogo bila kusahau unywaji maji ya kutosha. Kufanya hivi kutakusaidia kuweza kupungua na kuwa na mwili wa kawaida
5. kupata usingizi wa kutosha
Inashauriwa kulala masaa 6 hadi 8, kwani Kutopata usingizi wa kutosha hufanya mwili wako kumenโgenya chakula taratibu .
Lakini pia diet tu haitoshi mazoezi nayo ni muhimu katika kupunguza uzito,hakikisha unafanya mazoezi walau mara tatu hadi nne kwa week kwa muda wa dakika 20 hadi 30.
Please log in or register to leave a comment or reply.
Related Posts
Kichomi ni moja ya dalili za ugonjwa moyo. Kupatwa kichomi mara moja moja si vibaya.
Ukipatw...
Read More
Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba...
Read More
Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo ku...
Read More
Ukwaju ni tunda maarufu sana ambalo hupatikana katika maeneo yenye uoto wa kitropiki. Kwa kingere...
Read More
Faida kuu za ukwaju ni kama ifuatavyo:
Huondoa sumu Mwilini
Chanzo kizuri cha viua ...
Read More
Wakati wa kufanya tendo la ndoa wapo baadhi ya watu hupatwa na maumivu wakati au baada ya kushiriki ...
Read More
Kuamka asubuhi na mapema hupunguza uwezekano wa mwanamke kupata saratani ya matiti.
Kulinga...
Read More
Fangasi ya ukeni husababishwa na fangasi aina ya Candida albicans. Ugonjwa huu huitwa vaginal can...
Read More
Naamini umeshawahi kusikia kuhusu changamoto ya uvimbe kwenye kizazi kwa Wanawake yaani Fibroids....
Read More
Unahitaji vitu vifuatavyo:
a)Binzari ya unga
b)Maziwa fresh
c)Asali
d)Baku...
Read More
Zifutazo ni faida zitokanazo na ulaji wa tende;
1. Tende huongeza nguvu kutokana na kuwa na sukari ...
Read More
Tafadhali chukua walau dk 2 kusoma hii:
1. Chukulia ni muda wa saa 1:25 jion unarudi nyumba...
Read More
No comments yet. Be the first to share your thoughts!