Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Kuhamasisha Furaha na Uchangamfu katika Familia Yako

Kuhamasisha Furaha na Uchangamfu katika Familia Yako

Kuhamasisha Furaha na Uchangamfu katika Familia Yako

Familia nzuri ni ile ambayo inajumuis... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufanya Familia Iwe na Amani na Furaha

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufanya Familia Iwe na Amani na Furaha

Familia ni kitovu cha maisha yetu na ndiyo mahali ambapo tunapata faraja, amani na upendo. Kuwa n... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufurahia Kila Siku katika Familia Yako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kufurahia Kila Siku katika Familia Yako

Kuwa na familia yenye ushirikiano na furaha ni jambo muhimu sana katika maisha. Kwa kufanya hivyo... Read More

Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Vidokezo vya Kuonyesha Shukrani kwa Msichana Wako

Kumwonyesha shukrani msichana wako ni njia moja ya kumfanya ajisikie muhimu na kupendwa. Kwa hiyo... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu hisia na mahitaji yako

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu hisia na mahitaji yako

Kuwasiliana kwa ufanisi kuhusu hisia na mahitaji yako ni muhimu sana katika uhusiano. Hapa kuna mwon... Read More
Jukumu la Wazazi katika Kuwalea Watoto: Mawazo na Mazoea Bora ya Familia

Jukumu la Wazazi katika Kuwalea Watoto: Mawazo na Mazoea Bora ya Familia

Karibu kwenye mada hii muhimu ya jukumu la wazazi katika kuwalea watoto. Leo tutazungumzia mawazo... Read More

Njia za Kuleta Utendaji Bora katika Kufanya Mapenzi: Ushauri na Mazoezi

Njia za Kuleta Utendaji Bora katika Kufanya Mapenzi: Ushauri na Mazoezi

Leo hii, tunataka kuzungumzia kuhusu njia bora za kuleta utendaji bora katika kufanya mapenzi. Kw... Read More

Jinsi ya kuweka malengo na ndoto za pamoja na mke wako

Jinsi ya kuweka malengo na ndoto za pamoja na mke wako

Kuweka malengo na ndoto za pamoja na mke wako ni njia nzuri ya kuimarisha uhusiano na kujenga mwelek... Read More
Njia za Kuimarisha Heshima na Kusaidia Familia Iwe na Amani na Furaha

Njia za Kuimarisha Heshima na Kusaidia Familia Iwe na Amani na Furaha

  1. Kutumia mawasiliano mazuri na wapendwa wako ili kuimarisha uhusiano kati yenu. Hakikish... Read More

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Ushirikiano wa Kijamii na Familia katika Mahusiano

Kuimarisha ushirikiano wa kijamii na familia ni muhimu sana katika kuendeleza mahusiano yenye fur... Read More

Jinsi ya Kuishi kwa Amani na Ndugu: Kuepuka Migogoro na Kutunza Uhusiano

Jinsi ya Kuishi kwa Amani na Ndugu: Kuepuka Migogoro na Kutunza Uhusiano

  1. Jifunze kuwasiliana: Mawasiliano ni ufunguo wa uhusiano mzuri. Hakikisha unawasiliana k... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako

  1. Kukabiliana na Mazoea ya Kutokuwa na Ushirikiano na Kutoelewana katika Familia Yako
  2. Read More
πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About