Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Mambo ya kuzingatia kuhusu ugonjwa wa Kaswende

Featured Image
Kaswende husababishwa na bakteria aitwaye Treponema pallidum , ambaye pia huitwa spirochetes kutokana na umbo lake la mzunguko. Viumbe hawa hujipenyeza kwenye ngozi laini inayotanda midomo au sehemu nyeti. Yafuatayo ni mambo Muhimu ambayo unapaswa kuyafahamu kuhusu Ugonjwa wa Kaswende.

Jinsi ugonjwa wa Kaswende unavyoonea

Ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi. Kaswende haiambukizi kwa kuchangia vyoo, vitasa vya milango, mabwawa ya kuogelea, kuchangia nguo au vyombo vya chakula.

Kwa njia ya Kujamiiana

Kaswende ni ugonjwa unaoambukiza haraka sana, mara nyingi huambikizwa kupitia ngono. Kwa sababu ugonjwa huu huenezwa kwa kugusa moja kwa moja mchubuko wa kaswende (syphilitic sore) uliopo kwenye ngozi, njia kuu ya kuenea ni kupitia ngono ya kawaida, ya kutumia midomo na ile ya kinyume na maumbile.

Kwa njia ya kugusana Miili

Mara chache ugonjwa huu huweza kuambukiza kwa kubusiana au kugusana miili. Pamoja na kuwa ugonjwa huambukiza kupitia michubuko, mara nyingi michubuko hatarishi haitambulikani. Mtu aliyeambukizwa huwa hajielewi na hivyo kumwambukiza mpenzi wake.

Kwa mtoto kipindi cha ujauzito

Mwanamke mwenye mimba na ugonjwa huu anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni kupitia placenta au wakati wa kuzaliwa. Aina hii ya kaswende huitwa congenital syphilis, na inaweza kusababisha kujifungua mtoto mfu au mtoto akafa muda mfupi baada ya kuzaliwa. Watoto wengi hawaonyeshi dalili wanapozaliwa. Baadaye watoto huota vijipele, hupata matatizo ya meno, na kubonyea kwa mfupa wa pua – hali inayoitwa saddle nose, kuwa viziwi, kuwa na watoto wa jicho na kifafa.

Hatua za Kaswende

Ugonjwa wa kaswende hugawanywa katika hatua na kila hatua ikiwa na dalili tofauti, lakini wakati mwingine hakuna dalili zitakazojitokeza kwa miaka mingi. Uambukizaji unatokea kwenye hatua ya kwanza, ya pili na mara chache mwanzoni mwa hatua ya latent phase.

Hatua Ya kwanza Ya Kaswende – Primary Syphilis

Kaswende huanza kama mchubuko mmoja (au zaidi ya mmoja) mgumu usio na maumivu unaojulikana kama chancre kwenye sehemu za siri, kwenye mdomo, au kwenye ngoz,i siku 10-90 (wastani wa miezi 3) baada ya maambukizi. Mchubuko huu unaweza kubaki hapo bila kuleta usumbufu kwa kipindi kirefu na hata maiaka mingi. Mchubuko huu wa mviringo hutokea kwenye eneo la maambuikizi. Hata bila ya tiba yo yote, mchubuko huu unaweza ukapona wenyewe bila kuacha kovu katika wiki sita.

Hatua Ya Pili Ya Kaswende – Secondary Syphilis

Hatua ya pili inaweza ikadumu kwa mwezi mmoja hadi miezi sita ikianza kama wiki sita hadi miezi sita baada ya maambukizi. Dalili Katika hatua ya pili, vijipele huota mara nyingi vikianzia mgongoni na kuenea mwili mzima, pamoja na kwenye viganja vya mikono na kwenye nyayo. Vijipele hivi huwa vya mviringo vyenye rangi nyekundu au vyenye wekundu wa kahawia. Michubuko inayofanana na chunjua hutokea kwenye sehemu za midomo na mkundu. Vile kutatokea maumivu ya misuli, homa, kukauka koo, kuvimba tezi, kupunyuka nywele, kukonda na uchovu wa mwili. Latent Syphilis Kama tiba ya kaswende ya hatua ya pili haitatolewa, ugonjwa utaendelea kwenye hatua iitwayo latent stage. Katika hatua hii inayoweza kudumu kwa miaka kadhaa, mwili utautunza ugonjwa bila kuonyesha dalili zo zote. Pamoja na kuwa hakuna dalili zo zote zitakazoonekana, ugonjwa huu unaweza kuendelea kwenye hatua ya mwisho.

Hatua Ya Tatu Ya Kaswende – Tertiary syphilis

Asilimia 15 ya watu ambao hawakupata tiba kwenye hatua ya pili ya kaswende watapata kaswende ya hatua ya tatu – tertiary syphilis. Hatua hii inatokea miaka 10 hadi 30 baada ya dalili za mwanzo za kaswende. Dalili Dalili za kaswende za hatua hii ni pamoja na kushindwa kumudu matumizi ya viungo vya mwili, ganzi, upofu, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, madhara kwenye moyo na mishipa ya damu, madhara kwenye ini, mifupa na maungio ya mifupa. Kifo huweza kutokea kutokana na uharibifu wa viungo vya mwili.

Matibabu ya ugonjwa wa Kaswende

Ugonjwa wa kaswende unatibika. Kuwahi kumpa tiba mgonjwa wa kaswende ni muhimu kwani kuchelewa kunaweza kumletea madhara makubwa ya mwili au kifo. Kama ugonjwa haujazidi mwaka mmoja, mara nyingi dozi moja ya ya penicillin hutosha. Kaswende iliyoendelea kwenye hatua nyingine, dozi nyingine zitahitajika.
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Matumizi ya zabibu kavu kutibu shinikizo la chini la damu

Matumizi ya zabibu kavu kutibu shinikizo la chini la damu

Zabibu huweza kutumika kama tiba ya shinikizo la chini la damu kama ifuatavyo

1. Chukua za... Read More

Mambo 8 ya kushangaza yanayofanywa na mwili wako kukulinda pasipo wewe kujua

Mambo 8 ya kushangaza yanayofanywa na mwili wako kukulinda pasipo wewe kujua

Mwili wa binadamu unafanya mambo
mengi ya kibaiolojia ambayo mara
nyingi ni vigumu kuya... Read More

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Matumizi ya karoti na asali kutibu presha ya kushuka

Hatua za kufuata

1. Tengeneza glasi moja ya juisi ya karoti

2. ... Read More

Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Jinsi ya kujua kama una Mimba: Dalili za kwanza kabisa za Ujauzito

Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wak... Read More

Sababu ya meno kubadilika rangi

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao y... Read More

Jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia ugonjwa wa moyo

Jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia ugonjwa wa moyo

Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu ku... Read More

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Mambo ya Muhimu kufahamu kuhusu tatizo la mgongo wazi

Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (m... Read More

Faida za mnyonyo na mazao yake

Faida za mnyonyo na mazao yake

Nyonyo Mbarika (Castor)
Mnyony(KiSwahili) Erand (KiHindi) Kastorka(KiRusi) ni mmea wa jamii ... Read More

Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Matumizi ya tunda la shelisheli kama dawa ya ngozi

Shelisheli lililokomaa huwa na uzito wa hadi kilo 6, ambapo mshelisheli unaweza kukua kwa urefu w... Read More

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Faida 25 za kutembea kwa Miguu

Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili mfumo wa maisha ya watu pamoja na kuathiri afya zao kw... Read More
Madhara ya kunywa soda

Madhara ya kunywa soda

Tafiti zinasema kwamba mtu mmoja anayekunywa soda moja kwa siku, anakunywa zaidi ya galoni au dum... Read More

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia mvuke

Mvuke husaidia kusafisha ngozi. Ni rahisi sana kutumia mvuke kutibu chunusi.

Chemsha maji k... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About