Log in to access your menu with tools for managing π tasks, π₯ clients, π° finances, π learning, π personal growth, and π spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 17:04:20 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nimekuja kwa Rafiki angu kumtembelea kaacha maji jikon yeye kaenda kununua unga. Huku mm nikaongeza maji pale jikon. Kumbe yy aliweka maji saiz ya unga wake peke ykeβ¦ Sasa hiv TUNAKUNYWA UJI hata hatuongeleshani. Kimbelembele changu kimeniponza.. ππππ
Updated at: 2024-05-25 17:13:21 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
UNATOKA SEBULENI UNAENDA ZAKO CHOONI UNAINGIA TU HIVI GHAFLA UNAKUTANA NA MZIGO MKUBWA WA MAVI JUU YA CHOO ALAFU UNAAMUA KURUDI ZAKO ILE UNATOKA TU UNAMUONA DEMU MZURI ULIYEMTONGOZA JANA ANAKUJA KUINGIA CHOO ULICHOTOKA WW NA KINA MZIGO WA MAVI JUU NA AMEKUONA WW NDIO UMETOKA MLE NDANI ..unaamua kurudi ili uka flash bahat mby maji hakuna.!!!
πππHAPO NDIO UTAJUA KWANINI SIKU HIZI HATUPENDI UJINGAππππ
Updated at: 2024-05-25 17:54:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na hayaβ¦
1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani 2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio 3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban 4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule) 5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia "Ahaa eeh utaona sa nne" 6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao 7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika 8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki 9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwibaπ 10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo 11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa 12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake 13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule 14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peniπ 15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati 16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mboleaπ π Dah shule zetu hizi kiboko!!
Updated at: 2024-05-25 18:11:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hii ndio Bongo
Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.
MZEE: Chagua gari unalotaka mpenziβ¦.kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .
BINTI: Mi naitaka hii
MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee
MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lakoβ¦
Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.
MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.
Updated at: 2024-05-25 17:11:57 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MZARAMO V/S MCHAGA. Mzaramo alitangaza anatibu magonjwa yooooooote kwa tsh. 100,000/= Na kama akishindwa kukutibu anakurudishia laki yako nakukuongeza laki nyingine. MCHAGA akaona hii fursa yakujipatia hela aiwezi mpita akaenda kutibiwa. MZARAMO: "unaumwa nini?" MCHAGA: "Sisikii ladha ya aina yoyote mdomoni kabisaaaa.." MZARAMO: "sawa, toa laki kabisa.." Mchaga akatoa. MZARAMO akamuagiza msaidizi wake; "Naomba kikopo no.27 mpe anywe huyu.." MCHAGA akanywa akatema faster; "Puh puu puu, Aisee huu si mkojo huu..?" MZARAMO: "Umepona karibu tena.." Mchaga aka-mind sana Kesho yake akarudi tena hakuamini ameliwa pesa yake. MCHAGA: aisee nina tatizo la kumbukumbu nasahau sanaaaaa.." MZARAMO akamwambia "hakuna tabu, toa laki tukupe tiba..' MCHAGA akatoa pesa akijua leo lazima afanikiwe..' MZARAMO: "nesi naomba kikopo no.27.." MCHAGA: "ASA CHALII ANGU HICHO SI CHA JANA CHA MKOJO HICHO AISEE..?" MZARAMO: "UMEPONA KUMBUKUMBU UNAYO.
Updated at: 2024-05-25 17:07:36 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
SWALI: Nini maana ya matatizo..?
JIBU: matatizo ni pale unapopewa adhabu na mwanajeshi then akakuruhusu uondoke, lakini ukarukia pikipiki yako halafu ukapayuka..!!!!!Β Mwanajeshi, wee boya Tu