Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Jinsi ya kuongeza mvuto kwa mpenzi wako

Featured Image

Kama umeshushwa thamani unakuwa kwenye hatari ya kuachwa. Hata kama mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka. Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.

UNAFANYAJE SASA?

Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.

Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO

Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO

Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.

Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.

Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.

Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Ukumbuke kwamba, ukipata matatizo yoyote – binafsi au yanayosababishwa na uhusiano wenu, anakuwa hana uwajibikaji wa asilimia kubwa kwa tatizo hilo. Utabaki wewe na matatizo yako!

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Jinsi ya Kufanya Maamuzi ya Familia yanayofaa: Vidokezo na Mbinu Bora

Jinsi ya Kufanya Maamuzi ya Familia yanayofaa: Vidokezo na Mbinu Bora

Karibu katika mwongozo wetu wa jinsi ya kufanya maamuzi ya familia yanayofaa. Kama unavyojua, fam... Read More

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo ya haramu katika ngono/kufanya mapenzi? Hili ni swali ambalo linaweza kuwa na maji... Read More

Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Mahaba kwa wanawake wa siku hizi

Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo ... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho

Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu maadili na imani za kiroho ni muhimu katika kujenga uelewa na hesh... Read More
Jinsi ya Kupanga Tarehe ya Kipekee na Msichana Wako

Jinsi ya Kupanga Tarehe ya Kipekee na Msichana Wako

Jinsi ya Kupanga Tarehe ya Kipekee na Msichana Wako

Kupanga tarehe ya kipekee na msichana ... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima na Kujenga Amani na Furaha katika Familia

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima na Kujenga Amani na Furaha katika Familia

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Heshima na Kujenga Amani na Furaha katika Familia

Familia ... Read More

Njia za Kupunguza Mafadhaiko na Kukabiliana na Shinikizo katika Mahusiano

Njia za Kupunguza Mafadhaiko na Kukabiliana na Shinikizo katika Mahusiano

Mahusiano ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu. Hata hivyo, mara nyingi huleta mafadhaiko na shin... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano na marafiki

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kujenga na kudumisha uhusiano na marafiki

  1. Kuwa Mchangamfu Katika kujenga na kudumisha uhusiano na marafiki, ni muhimu kuwa mchang... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu njia za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu njia za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu sana kwenye makala hii ya blog, ambapo tutajadili kuhusu kwa nini watu wanapendelea kutafu... Read More

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano na Ushirikiano wa Familia katika Mirathi na Mali

Jinsi ya Kukuza Ushirikiano na Ushirikiano wa Familia katika Mirathi na Mali

Kujenga ushirikiano na ushirikiano wa familia katika mirathi na mali ni muhimu kwa maendeleo ya f... Read More

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha Ushirikiano wa Kifedha na Kuweka Malengo ya Pamoja katika Familia

Kuhamasisha ushirikiano wa kifedha na kuweka malengo ya pamoja katika familia ni muhimu sana kati... Read More

Je, ni muhimu kuwa na usawa wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Je, ni muhimu kuwa na usawa wa ngono/kufanya mapenzi katika uhusiano?

Habari za leo wapenzi! Sijui kama umewahi kujiuliza kuhusu umuhimu wa usawa wa ngono/kufanya mape... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About