Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Featured Image

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna umuhimu wa kujadili mawazo na hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili mawazo na hisia wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Kwa wengi, ngono inaonekana kama kitendo cha kimwili tu bila ya umuhimu wa kujadili mawazo na his... Read More

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu uwekezaji na mipango ya fedha ya baadaye

Jinsi ya Kusaidiana na mpenzi wako katika kufanya maamuzi muhimu kuhusu uwekezaji na mipango ya fedha ya baadaye

Mahusiano ya kimapenzi huwa yanahitaji ushirikiano wa pamoja kwa ajili ya kuweza kufanikiwa. Ni m... Read More

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya burudani na michezo

Jinsi ya Kuwasiliana na mpenzi wako kuhusu masuala ya burudani na michezo

Kuwasiliana na mpenzi wako ni muhimu sana ili kudumisha uhusiano wenye afya na furaha. Kuna mambo... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazoea ya Kijamii yenye Msaada katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuwa na Mazoea ya Kijamii yenye Msaada katika Ndoa na mke wako

Kuwa na mazoea ya kijamii yenye msaada katika ndoa na mke wako ni muhimu kwa kujenga uhusiano wa kar... Read More
Kuimarisha Uhusiano kupitia Mazoezi ya Kimwili: Kufanya Mapenzi kama Njia ya Kujenga Ushirikiano

Kuimarisha Uhusiano kupitia Mazoezi ya Kimwili: Kufanya Mapenzi kama Njia ya Kujenga Ushirikiano

  1. Kufanya mazoezi pamoja na mwenzi wako ni njia bora ya kuimarisha uhusiano wenu na kuongeza ... Read More
Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Ushirikiano katika Familia

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Ushirikiano katika Familia

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Ushirikiano katika Familia

Familia ni kiini cha jamii,... Read More

Njia za Kuimarisha Heshima na Uthamani katika Mahusiano

Njia za Kuimarisha Heshima na Uthamani katika Mahusiano

Heshima na uthamani ni mambo muhimu sana katika mahusiano, kwani yanajenga msingi thabiti wa upen... Read More

Jinsi ya Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako

Jinsi ya Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako

Kuweka mipango ya likizo na mapumziko pamoja na mpenzi wako ni njia nzuri ya kujenga uhusiano thabit... Read More
Mwanamme: Mbinu za Kukua na Kupata Maendeleo Na kukabiliana na matatizo ya Kiuchumi

Mwanamme: Mbinu za Kukua na Kupata Maendeleo Na kukabiliana na matatizo ya Kiuchumi

Read More
Vidokezo vya Kufurahia Safari za Pamoja na Msichana

Vidokezo vya Kufurahia Safari za Pamoja na Msichana

Kila mwanamume anapenda kukutana na msichana ambaye anaweza kuwa rafiki wa karibu na kuwa na uhus... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa wazazi na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kuwa wazazi na mpenzi wako

Kuwa wazazi na mpenzi ni changamoto kubwa katika maisha yetu. Mawazo mengi yako kwenye familia na... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Uhusiano Wenye Furaha na Msichana

Kuwa na uhusiano wenye furaha na msichana ni jambo ambalo kila mwanaume anatamani. Lakini mara ny... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About