Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jifunze kitu kupitia kisa hiki cha mume na mke

Featured Image

Mwanaume mmoja alimuoa mwanamke mrembo. Alikuwa akimpenda sana. Siku moja mwanamke alipatwa na maradhi ya ngozi. Kidogokidogo alianza kupoteza urembo wake.
.
.
.

Mume alipata safari na wakati akirudi alipata ajali iliyomfanya apoteze uwezo wake wa kuona. Hata hivyo, maisha yao ya ndoa yaliendelea kama kawaida. Lakini kadiri siku zilivyosonga mbele ndivyo mke alivyoendelea kupoteza urembo wake. Kwa kuwa mume alikuwa kipofu hakulijua hilo na hivyo hakuna kilichobadilika kwenye upendo wao. Aliendelea kumpenda, na mke alimpenda sana mumewe.
.
.
.

Siku moja mke alifariki dunia. Ilikuwa huzuni kubwa sana kwa mume.
Baada ya kumaliza taratibu zote za maziko, mazishi na kutandua msiba, alipanga kuhama kwenye mji huo na kwenda kuishi kwenye mji mwingine.
.
.
.

Mtu mmoja aliposikia habari hiyo alimwendea na kumuuliza: โ€œSasa utawezaje kutembea peke yako? Maana siku zote hizi mkeo alikuwa akikusaidia kukuonesha njia.โ€

Akajibu: โ€œMimi si kipofu. Nilifanya ionekane hivyo kwa sababu angejua kwamba ninauona mwili wake ulivyobadilika kuwa mbaya angepata maumivu makubwa zaidi kuliko ugonjwa wake wenyewe. Alikuwa mke mwema sana. Nilitaka aendelee kuwa na furaha.โ€
.
.
.

FUNZO:

Wakati fulani ni vizuri ukajifanya kipofu na kuyapuuza mapungufu ya mwenzako ili kumfanya awe mwenye furaha.

Meno huungโ€™ata ulimi mara nyingi, lakini vinaendelea kuishi pamoja kinywani. Huo ndio moyo wa KUSAMEHEANA. Macho hayaonani, lakini yanatazama na kuona vitu kwa pamoja, hupepesa na kulia pamoja. Huo unaitwa UMOJA.

1. Ukiwa peke yako unaweza kuongea, lakini ukiwa pamoja na mwenzako mnaweza KUZUNGUMZA.

2. Ukiwa peke yako unaweza KUFURAHI, lakini ukiwa na mwenzako unaweza KUFURAHIA.

3. Ukiwa peke yako unaweza KUTABASAMU, lakini ukiwa na mwenzako mnaweza KUCHEKA.

Huo ndio UZURI wa mahusiano yetu kama binadamu. Tunategemeana.

Kiwembe kina ukali lakini hakiwezi kukata mti; shoka lina nguvu na imara lakini haliwezi kukata nywele.

*Kila mtu ni muhimu kulingana na kusudio na lengo la uwepo wake. Usimdharau mtu yeyote kwa hali yoyote, kwa sababu huwezi kuwa yeye.

Mwenyezi Mungu atujaalie nguvu na moyo wa kusamehe, kustahmiliana na kuishi kwa umoja.
.
Tafakari
Mm na ww tunaweza kufanya haya!!!

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki niย Soft copy [pdf]ย kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

[products columns="2" ids="30827"]
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kuweka Kipaumbele cha Ukaribu na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kila Mwanafamilia

Kuweka Kipaumbele cha Ukaribu na Kuunga Mkono Maendeleo ya Kila Mwanafamilia

Kuweka kipaumbele cha ukaribu na kuunga mkono maendeleo ya kila mwanafamilia ni jambo muhimu sana... Read More

Maadili na Kanuni za Familia: Mwongozo wa Kuishi Kwa Furaha

Maadili na Kanuni za Familia: Mwongozo wa Kuishi Kwa Furaha

  1. Familia ni moja ya nguzo kuu katika maisha yetu ya kila siku, na kwa hivyo ni muhimu sa... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazoea ya Kijamii yenye Msaada katika Ndoa na mke wako

Jinsi ya Kuwa na Mazoea ya Kijamii yenye Msaada katika Ndoa na mke wako

Kuwa na mazoea ya kijamii yenye msaada katika ndoa na mke wako ni muhimu kwa kujenga uhusiano wa kar... Read More
Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuwa na Amani na Furaha katika Familia yako

Njia za Kuimarisha Ushirikiano na Kuwa na Amani na Furaha katika Familia yako

  1. Kujenga mawasiliano ya wazi na familia yako: Ni muhimu kuwa na mawasiliano ya wazi na f... Read More

Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Ujuzi wa Kijamii na Kuwa na Ukaribu

Jinsi ya Kusaidia Watoto kujenga Ujuzi wa Kijamii na Kuwa na Ukaribu

Karibu kwenye makala yetu ya leo kuhusu jinsi ya kusaidia watoto kujenga ujuzi wa kijamii na kuwa... Read More

Kuweka Kipaumbele cha Kuimarisha Ushirikiano wa Kiroho katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Kuimarisha Ushirikiano wa Kiroho katika Familia Yako

Kuweka Kipaumbele cha Kuimarisha Ushirikiano wa Kiroho katika Familia Yako

Familia ni nguz... Read More

Njia za Kukuza Ushawishi wa Mwanamke katika Kufanya Mapenzi: Kuamsha Uwezo wa Kujiamini

Njia za Kukuza Ushawishi wa Mwanamke katika Kufanya Mapenzi: Kuamsha Uwezo wa Kujiamini

Kama mwanamke, unapambana na changamoto nyingi katika maisha yako ambazo zinaweza kukuzuia kufany... Read More

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mawasiliano katika Mahusiano: Kuunda Nafasi ya Mazungumzo

Kukabiliana na Mazoea ya Kukosa Mawasiliano katika Mahusiano: Kuunda Nafasi ya Mazungumzo

Mawasiliano ni muhimu sana katika mahusiano. Hata hivyo, kuna wakati tunapokumbana na changamoto ... Read More

Ushauri kuhusu mwanamke wa kufaa kuoa

Ushauri kuhusu mwanamke wa kufaa kuoa

Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu... Read More

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kujenga na Watoto: Kusikiliza na Kuelewa

Jinsi ya Kuwa na Mazungumzo ya Kujenga na Watoto: Kusikiliza na Kuelewa

Habari ndugu yangu! Umeamua kuchagua njia sahihi ya kuwa na mazungumzo ya kujenga na watoto wako.... Read More

Njia za Kuimarisha Ushawishi wa Kidiplomasia katika Mahusiano yako

Njia za Kuimarisha Ushawishi wa Kidiplomasia katika Mahusiano yako

Njia za Kuimarisha Ushawishi wa Kidiplomasia katika Mahusiano yako

Ushawishi wa kidiplomas... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kazi na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kazi na mpenzi wako

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na mabadiliko ya kazi na mpenzi wako

Wakati mwingine maish... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About