Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kwa nini wasichana wakiingia utu uzima damu zinaanza kutoka kwenye uke?

Featured Image
Kutoka damu (hedhi) kwa mara ya kwanza kunaitwa kuvunja ungo na hii ni dalili ya mtoto wa kike kuingia utu uzima,0 yaani kuwa mwanamke. Wasichana wanavunja ungo kati ya umri wa miaka 8 na umri wa miaka 18. Lakini, kuvunja ungo haina maana kwamba unahitaji kuanza kujamii ana. Kwa sababu ukijamii ana kuna hatari ya kupata mimba! Mwanzoni siku za hedhi zinaweza kuwa na mabadiliko sana. Ni baada ya muda ndipo msichana anaanza kwenda mwezini mara moja kila mwezi. Kwa wanawake wengi ni kila baada ya siku 28, hata hivyo, wengine huweza kupata hedhi chini au zaidi ya siku hizo. Idadi ya siku katika mzunguko wa hedhi ni siku 21 hadi 35.Ukitaka kuelewa kabisa maana ya kutoka damu za mwezi, lazima nieleze kuhusu mzunguko wa hedhi. Siku ya kwanza ya damu huhesabiwa kama siku ya kwanza ya mzunguko. Baada ya damu kutoka, yai moja linaanza kukua ndani ya kokwa. Na vilevile utando ndani ya mfuko wa uzazi huanza kujengeka ili ukaribishe mimba. Kati ya siku 11 au 14 yai hupevuka ndani ya kokwa na halafu husafiri kwenye mirija ya kupitishia mayai hadi kwenye mfuko wa uzazi. Mwanamke anapata mimba kama yai likirutubishwa na mbegu ya kiume ndani ya mirija ya kupitisha mayai, i ina maana, kwamba atakuwa amejamii ana kipindi cha siku chache kabla ya yai kupevuka au siku yai linapopevuka. Kama yai halikurutubishwa, basi hufa na hutangulia kutoka kama ute, pia utando kwenye mfuko wa uzazi na kuta za uzazi hubomoka na kutoka kama damu. Hii ndiyo hedhi yenyewe. Endapo msichana amejamiiana na mvulana na yai likarutubushwa, hataona hedhi na aelewe kwamba kuna uwezekano kwamba mimba imetungwa. Mzunguko wa hedhi kwa baadhi ya wasichana hauna mpangilio mwanzoni, hivyo endapo hupati hedhi inayolingana kila mwezi usijali. Katika hali ya kawaida usipopata hedhi na hukujamiiana na mvulana, basi inawezekana ni mabadiliko tu ya mwili. Hali hii ikiendelea au ukiwa na wasiwasi unashauriwa kumuona mtaalamu wa afya
AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Kufikia mshindo au kufika kileleni kwa mwanamke na mwanamme wakati wa kufanya mapenzi

Kufikia mshindo au kufika kileleni kwa mwanamke na mwanamme wakati wa kufanya mapenzi

Je, mwanamke anaweza kufikia mshindo?

Ndiyo, mwanamke anaweza kufikia mshindo wakati wa kuj... Read More
Ni asilimia ipi ya Watanzani ambao wameambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Ni asilimia ipi ya Watanzani ambao wameambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Nchini Tanzania ni 7% ya watu wenye umri kati ya miaka 15-49 wana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI... Read More

Je, ni kweli matumizi ya dawa za kulevya ni mojawapo ya sababu zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)

Je, ni kweli matumizi ya dawa za kulevya ni mojawapo ya sababu zinazochangia maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU)

Dawa za kulevya zenyewe hazisababishi UKIMWI na magonjwa ya zinaa. Lakini utumiaji wa dawa za kul... Read More

Madhara ya pombe kwa mwili na akili

Madhara ya pombe kwa mwili na akili

Pombe huingia kwenye damu na kuzunguka mwili mzima pamoja
na kwenye ubongo wako. Ina madhara... Read More

Mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI, anaweza kuzaa mtoto?

Mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI, anaweza kuzaa mtoto?

Na anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni au wakati wa kumnyonyesha?
Ndiyo, mama mwenye vi... Read More

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Inakuwaje mtoto anakuwa wa kike au wa kiume?

Mwili wa mwanaume unatengeneza aina mbili za mbegu. Kuna mbegu zinazokua kuwa mtoto wa kiume na k... Read More

Je, muda wa kufanya ngono/kufanya mapenzi ni muhimu?

Je, muda wa kufanya ngono/kufanya mapenzi ni muhimu?

Je, muda wa kufanya ngono/kufanya mapenzi ni muhimu? Hili ni swali ambalo huwa linawasumbua wapen... Read More

Ukeketaji ni nini?

Ukeketaji ni nini?

Katika baadhi za jamii viungo vya uzazi vya nje vya msichana,
yaani kisimi au sehemu ya ndan... Read More

Mafuta kwenye kondomu

Mafuta kwenye kondomu

Mafuta yanayowekwa kwenye pakiti ya kondomu ni mafuta maalum na yana kazi ya kuhifadhi kondomu mp... Read More

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya hisia na utambuzi katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kujadili masuala ya hisia na utambuzi katika uhusiano wa ngono/kufanya mapenzi?

Habari rafiki yangu! Leo tuzungumzie suala muhimu sana ambalo linapaswa kujadiliwa katika uhusian... Read More

Nifanyeje kuepuka vishawishi vya kujamiiana kutoka kwa watu wengine, hasa wakubwa?

Nifanyeje kuepuka vishawishi vya kujamiiana kutoka kwa watu wengine, hasa wakubwa?

Vijana wengi wanajikuta wanatumbukia katika matatizo mazito kama kupata mimba mapema, utoaji wa m... Read More

Kumbadilisha mtu aliyeathirika na dawa za kulevya

Kumbadilisha mtu aliyeathirika na dawa za kulevya

Endapo rafiki au jamaa anaomba msaada wa kuacha kutumia dawa za kulevya unaweza kumsaidia kwa kum... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About