Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE ๐Ÿ”
โ˜ฐ
AckyShine

Jinsi ya kutumia kondomu ya kike

Featured Image

Kondomu ya kike inafahamika kwa jina la โ€žcareโ€œ na โ€œLady Petetaโ€. Hapa Tanzania hazipatikani sehemu zote na bei yake ni kubwa kidogo.
Kondomu ya kike huingizwa ukeni kabla ya kujamiiana. Kama unatumia kondomu ya kike, chana kwa uangalifu pembezoni mwa pakiti. Kondomu ina pete mbili za plastiki na uwazi upande wa juu. Pete moja imelegea ni ndogo na iko kwa ndani, upande usio na uwazi. Pete ya pili ni kubwa zaidi, imeshikiliwa na iko upande wa tundu. Shikilia kondomu upande uliozibwa na minya pete ya ndani kwa dole gumba na kidole cha pili na cha kati. Mara nyingine inaweza ikakuponyoka, (kuteleza) lakini endelea kujaribu hadi umeiminya vizuri. Tafuta mkao mzuri na ingiza kondomu ya kike. Huku bado unaminya kwa vidole vyako iongoze kondomu ndani ya uke wako. Ukiiachia pete ya ndani itashikilia kondomu ndani ya uke. Sasa ingiza kidole chako kwenye kondomu, sukuma pete mpaka inapogota kwenye mlango wa uzazi.
Kondomu ya kike inaweza kuvaliwa saa kadhaa kabla ya kufanya ngono na pia inaweza kuvuliwa baada ya muda wa kufanyika ngono kupita. Ili kuhakikisha kuwa uume umeingia sehemu husika, msaidie mwenzi wako kuongoza uume kuingia kwenye uke ili usipenye pembeni.
Baada ya kujamiiana, vua kondomu kwa uangalifu. Tupa kondomu iliyotumika kwenye choo cha shimo au uichome. Usitupe kondomu iliyotumika ovyo.
Kama ilivyo kwa kondomu ya kiume, kondomu ya kike itatumika kwa mafanikio zaidi pale ambapo wahusikia wanakuwa na makubaliano na maelewano juu ya matumizi yake.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Nifanyeje Kuzungumzia Suala la Kukosa Hamu ya Ngono?

Nifanyeje Kuzungumzia Suala la Kukosa Hamu ya Ngono?

Nifanyeje Kuzungumzia Suala la Kukosa Hamu ya Ngono? ๐Ÿ˜Š

  1. Jambo la kwanza kabisa... Read More

Je, kuna mambo mazuri na mabaya kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo mazuri na mabaya kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna mambo mazuri na mabaya kuhusu ngono/kufanya mapenzi? Ndio, kuna mambo mengi sana ambayo ... Read More

Je, mtu anawezaje kuacha kutumia dawa za kulevya na itamchukua muda gani kurudia hali yake ya kawaida?

Je, mtu anawezaje kuacha kutumia dawa za kulevya na itamchukua muda gani kurudia hali yake ya kawaida?

Kitu muhimu ni kwamba, kweli uwe umedhamiria kuacha. Hatua ya kwanza ni kujiuliza kwa nini unatum... Read More

Je, pombe inaweza kusababisha uitegemee?

Je, pombe inaweza kusababisha uitegemee?

Ndiyo, Kama nikotini, pombe huweza kukufanya mwenye busara
iwapo utakunywa, na ujiwekee kiwa... Read More

Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

Je, kuna madhara gani usipooga baada ya kujamiiana?

Hakuna madhara yoyote ya msingi anayopata mtu asipooga baada ya kujamiiana. Isipokuwa kwa ajili y... Read More

Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?

Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?

Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa... Read More
Je, ni sahihi kuzungumza na wenzio/ marafiki juu ya uhusiano wangu wa kimapenzi?

Je, ni sahihi kuzungumza na wenzio/ marafiki juu ya uhusiano wangu wa kimapenzi?

Kama unavyohusisha rafiki zako katika mihemuko mingine, inaeleweka kama utataka kuwashirikisha ka... Read More

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Ipo njia moja ya kuhakikisha kama umeambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI au hapana. Njia hii ni... Read More

Je, kuwa kuna mambo ambayo hayafai kuzungumziwa kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuwa kuna mambo ambayo hayafai kuzungumziwa kuhusu ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako, mpenzi! Katika mada ya leo, tunajadili kuhusu mambo ambayo hayafai kuzungumziwa kuhu... Read More

Je, unaweza kupanga kuzaa aina ya watoto, yaani wa kiume au wa kike tu?

Je, unaweza kupanga kuzaa aina ya watoto, yaani wa kiume au wa kike tu?

Mimba i inatungwa wakati yai la kike linaporutubishwa na mbegu za kiume. Kama tulivyoona hapo juu... Read More

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Ushauri kwa mtu aliyebakwa

Jambo la kwanza jaribu kumwondoa hofu mwathiriwa na
muliwaze maana amepata jambo la kutisha.... Read More

Haki za ujinsia na afya ya uzazi zinamhusu pia mtu anayeishi na ualbino?

Haki za ujinsia na afya ya uzazi zinamhusu pia mtu anayeishi na ualbino?

Haki za msingi; hasa zile zinazohusiana na kuthaminiwa na
kuheshimiwa kama binadamu zinawahu... Read More

๐Ÿ“– Explore More Articles
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About