Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Je, kwa nini akina mama wajawazito hawatakiwi kunywa pombe?

Featured Image

Wanawake wajawazito ambao hunywa pombe au kuvuta sigara
wanahatarisha afya na maisha ya mtoto aliye tumboni. Mtoto aliye
tumboni hurutubishwa kupitia damu ya mama. Kama mama atavuta
sigara au kunywa pombe, sumu illiyopo katika sigara au pombe
inapoingia kwenye damu yake itamfikia mtoto pia. Pombe hushambulia
moyo uendeleao kukua na ubongo wa mtoto aliye tumboni.
Akina mama wanaokunywa kupita kiasi wakiwa wajawazito
wanaweza kupata watoto wenye magonjwa ya moyo au mtindio
wa akili, kwa sababu chembechembe za ubongo hazikui vizuri.
Mara nyingi watoto huzaliwa na upungufu katika mwonekano
wa sura. Kwa mtoto pombe ni sumu kali, hata kama ni kwa kiasi
kidogo, itamdhuru.

Mama anaekunywa pombe anaweza kuwa hajali au kusahau
kujilinda mwili wake na mtoto anayekua.
Kama akipata maambukizo ya VVU na mtoto pia anaweza
akapata virusi vya UKIMWI.
Wanawake wanaovuta sigara wakiwa wajawazito wana
uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto ambao hufariki ghafla bila
sababu ya kueleweka katika mwaka wao wa kwanza wa maisha.
Watoto wa akina mama wanaovuta sigara mara nyingi huzaliwa
na umbo dogo kuliko wengine kwa sababu watoto walipata
chakula kidogo walipokuwa bado tumboni mwa mama zao.
Ujumbe upo wazi: Wanawake wanaotaka watoto wenye afya
wasivute kabisa sigara wala kunywa pombe wakiwa wajawazito.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

No comments yet. Be the first to share your thoughts!

Related Posts

Je, kuna umuhimu wa kuwa na uelewa wa afya ya uzazi na uzazi katika ngono/kufanya mapenzi?

Je, kuna umuhimu wa kuwa na uelewa wa afya ya uzazi na uzazi katika ngono/kufanya mapenzi?

Habari yako rafiki! Leo, ningependa kuzungumza nawe kuhusu umuhimu wa kuwa na uelewa wa afya ya u... Read More

Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?

Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?

Tunatofautisha dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile zisizokubalika ... Read More

Kwa nini ngozi ya Albino inafanana ya watu weupe?

Kwa nini ngozi ya Albino inafanana ya watu weupe?

Ngozi ya Albino ina ukosefu wa rangi. Inaonekana kama ya watu
weupe ambao wana kiasi cha pig... Read More

Kama watu wanataka kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe wafanyeje?

Kama watu wanataka kuacha kuvuta sigara au kunywa pombe wafanyeje?

Kwanza kabisa, watu ni kweli wawe wamedhamiria kuacha. Hii inataka uamuzi wa wazi na nia imara kwa s... Read More
Je, nini kitatokea iwapo mwanamke atatumia dawa za kulevya wakati wa ujauzito?

Je, nini kitatokea iwapo mwanamke atatumia dawa za kulevya wakati wa ujauzito?

Kama mama mjamzito atatumia dawa za kulevya basi humuathiri mtoto moja kwa moja. Mtoto aliye tumb... Read More

Njia za Kudumisha Mapenzi katika Uhusiano wako na Msichana

Njia za Kudumisha Mapenzi katika Uhusiano wako na Msichana

Mapenzi ni muhimu katika uhusiano wowote wa kimapenzi. Ni muhimu kuchukua hatua za kudumisha mape... Read More

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Vidokezo vya Kuwa na Mazungumzo ya Kina na Msichana

Kama kijana, kuna wakati unaweza kukutana na msichana na unataka kuzungumza naye kwa kina lakini ... Read More

Vidokezo vya Kujenga Ukaribu na Msichana Wako

Vidokezo vya Kujenga Ukaribu na Msichana Wako

  1. Anza kwa kujenga urafiki mzuri Kabla ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi, ni muhimu kujeng... Read More

Jinsi ya kutumia Kondomu

Jinsi ya kutumia Kondomu

Wakati wa kutumia kondomu ya kiume ni muhimu kufuata hatua zifuatazo. Hakikisha kwamba pakiti ina... Read More

Vidokezo vya Kuepuka Mazungumzo ya Kuchosha na Msichana

Vidokezo vya Kuepuka Mazungumzo ya Kuchosha na Msichana

Mazungumzo ni sehemu muhimu katika uhusiano wowote wa kimapenzi. Lakini kuna wakati mazungumzo ya... Read More

Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali

Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali

Jinsi ya Kupata Msichana wa Kuwa na Uhusiano wa Mbali

Kuwa na uhusiano wa mbali sio rahisi... Read More

Kwa nini dawa hutengenezwa na kutumika hospitalini wakati zina madhara?

Kwa nini dawa hutengenezwa na kutumika hospitalini wakati zina madhara?

Baadhi ya dawa za kulevya pamoja na dawa za kutibu, hutumika hospitali kuokoa maisha na kupunguza... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About