Warning: Undefined variable $user_id in /home/ackyshine/personal/sidebar.php on line 36
Sidebar with Floating Button
AckySHINE πŸ”
☰
AckyShine

Kisa cha kusisimua: Funzo kwa mabinti

Featured Image

Kijana maskini na mwenye maisha duni alimpenda msichana mmoja
Baada ya kutumia muda mwingi kumfikiria msichana huyo,
Siku moja akaamua kumwita na kumwambia ukweli ya kwamba amempenda na angehitaji kumuoa.

Msichana kwa nyodo na jeuri akasema "sikiliza tena unisikilize kwa makini wewe maskini mshahara wako unaopokea kwa mwezi hautoshi hata kwa matumizi yangu ya siku moja sasa utawezaje kunitunza mm!

Kwaufupi mm sio levo zako hivyo basi sahau kabisa kuhusu kunipata mimi
Nenda katafute maskini mwenzio atakae endana na maisha yako,
Mwisho akamwangalia kwa dharau na kisha akaenda zake.

Kwanzia siku ile kijana hakubahatika tena kumuona msichana yule lkn kwakuwa alimpenda basi hakuweza kumsahau kirahisi rahisi siku zilienda na miezi ikasonga,
Miaka 10 baadae wawili hawa walikuja kukutana katika supermarket moja hivi mjini

Kijana alipomwona msichana alitabasamu lakin kabla hajasema chochote msichana kama kawaida yake kwa dharau akasema "we maskin upo! hivi na ww unaingiaga supermarket eh!

Akaongeza huku akisema walau sasahivi nakuona umependeza inaonekana boss wako kakuongeza mshahara
ila kwa kifupi naomba nikwambie sasahivi nimeshaolewa mume wangu anafanya kazi kwenye kampuni moja hivi ya mtu binafsi kampuni maarufu sana na mshahara wa mume wangu ni shilingi milioni moja na laki mbili kwa mwezi na malupulupu mengine kibao,
Unafikiri ww na umaskini wako kuna siku utakuja kufikia kiwango cha mshahara anachopokea mume wangu!

Macho ya kijana yalitokwa na machozi kwa kuona msichana hajabadilika na anaendelea kuwa na maneno ya kejeri na dharau.

Mara hii mume wa yule dada akaingia ktk supermarket
Ile kumuona yule kijana mume akasema "ooh! Kiongozi upo hapa! Leo imekuwa bahati umekutana na mke wangu!" Kisha akamgeukia mke wake na kusema "mke wangu huyu ndo boss wangu

Na unajua nn mke wangu usishangae kumuona boss wangu anakuja kununua vitu mwenyewe hapa supermarket ukweli ni kwamba boss wangu hana mke, anasema alisha wahi kumpenda msichana mmoja lakini hakufanikiwa kumpata na amekuwa na ndoto ya kuja kukutana tena na msichana huyo ndio maana mpaka sasa bado hajaoa.

Akaendelea kusema hebu fikiria ni bahati kiasi gani alikuwa nayo msichana huyo kama angekubali kuolewa na boss wangu leo hii siangekuwa
maisha!

Muda wote msichana alikuwa kimya hajui hata ajibu nn kwa dharau alizomuonyesha kijana tangu mwanzo.


UJUMBE WANGU
Kwenye maisha mambo huweza kubadilika kama vile upepo unavoweza kubadili mwelekeo kulingana na masaa Hivyo basi usimdharau na kumbeza mtu yeyote kwa sababu ya hali aliyonayo,
Maana kila mtu anafungu lake alilopangiwa na Mungu,

Lakini pia kumbuka hakuna ajuaye kesho
Wakati mwingine mtu unayemdharau leo ndiye huyohuyo ambaye kesho utasimulia mafanikio yake.

Kwako unayesoma ujumbe huu nakuombea Mungu akakufungulie milango ya baraka na kuyapa thamani maisha yako ili pale ulipozomewa ukashangiliwe na wale wote waliokudharau punde wakapate kukupigia magoti kwa uweza wa Mungu.

AckySHINE Solutions

Comments

Please log in or register to leave a comment or reply.

Director J (User) on May 15, 2025

Good story πŸ’ͺ

Related Posts

Jinsi ya Kuwa na Furaha na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Furaha na Msichana Wako

Jinsi ya Kuwa na Furaha na Msichana Wako

Kuwepo kwa mtu ambaye unampenda na kujali ni jamb... Read More

Njia za Kuonyesha Msichana Wako Kuwa Ana thamani Kwako

Njia za Kuonyesha Msichana Wako Kuwa Ana thamani Kwako

Kama mwanaume, kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya ili kuonyesha msichana wako kuwa ana thama... Read More

Kuwa na msimamo katika mahusiano

Kuwa na msimamo katika mahusiano

Sio Kila EX Wako Anayeomba Mrudiane Anamaanisha! Wengine Huomba Kurudi Ili Wakutesti Tu Jinsi Uli... Read More

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuwa na Msamaha katika Mahusiano

Njia za Kupunguza Mazoea ya Kutokuwa na Msamaha katika Mahusiano

Mahusiano ni sehemu muhimu ya maisha ya binadamu, lakini mara nyingi tunaweza kuingia kwenye mazo... Read More

Kuweka Mazingira ya Upendo na Ukarimu katika Familia ili Kuwa na Amani na Furaha

Kuweka Mazingira ya Upendo na Ukarimu katika Familia ili Kuwa na Amani na Furaha

Kuweka mazingira ya upendo na ukarimu katika familia ni muhimu sana ili kuwa na amani na furaha. ... Read More

Jinsi ya Kuonyesha Upendo kwa Msichana Wako kila Siku

Jinsi ya Kuonyesha Upendo kwa Msichana Wako kila Siku

Wewe ni mpenzi mzuri na unapenda msichana wako kwa dhati. Lakini je, unamwonyesha upendo kila sik... Read More

Jinsi ya kusaidiana na mke wako katika afya na ustawi

Jinsi ya kusaidiana na mke wako katika afya na ustawi

Kusaidiana na mke wako katika afya na ustawi ni jambo muhimu katika kujenga ndoa yenye furaha na afy... Read More
Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, wasichana wanatofautiana ila w... Read More

Je, watu wanapendelea kujaribu njia za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Je, watu wanapendelea kujaribu njia za kuleta msisimko wakati wa ngono/kufanya mapenzi?

Karibu sana kwenye makala hii ya blog, ambapo tutajadili kuhusu kwa nini watu wanapendelea kutafu... Read More

Kuhamasisha Mazungumzo ya Kujamiiana katika Uhusiano: Kujenga Uwazi na Uwepo

Kuhamasisha Mazungumzo ya Kujamiiana katika Uhusiano: Kujenga Uwazi na Uwepo

Kuhamasisha Mazungumzo ya Kujamiiana katika Uhusiano: Kujenga Uwazi na Uwepo

Katika uhusia... Read More

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali wanyama

Jinsi ya Kuelewa na kukabiliana na changamoto za kusaidia na kuwajali wanyama

Kama mpenzi wa wanyama, tunajua jinsi inavyokuwa muhimu kuwasaidia na kuwajali. Lakini, kuna nyak... Read More

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Kuthamini katika Mahusiano yako

Kujenga Mazingira ya Ushirikiano na Kuthamini katika Mahusiano yako

Mahusiano ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu. Lakini ili kuyafanya yawe endelevu, ni muhimu kuw... Read More

πŸ“– Explore More Articles
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About