Maswali na Majibu kuhusu Mafumbo ndani ya Kanisa Katoliki
Welcome Back.
Updated at: 2024-05-27 06:45:12 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Updated at: 2024-05-27 06:45:28 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Tumeamriwa tuwaheshimu wazazi wetu na wakubwa wetu wote, tuwapende, tuwatii na tuwaombee. (Kut 20:12, Kol 3:20)
Tumeamriwa tuwaheshimu wazazi wetu na wakubwa wote, tuwapende, tuwatii na tuwaombee. (Kut 20:12), Kol 3:20
Yatupasa kuwaheshimu Baba na Mama kwa sababu;
1. Wameshirikiana na Mungu kutuleta duniani walipotuzaa
2. Wamewekwa na Mungu ili watulee na kutuongoza Mbinguni
3. Mungu ameamuru tuwapende wazazi mara baada ya Yeye. (Ayu 3:1-9)
Wazazi na wakubwa wameamriwa watutunze na kutulea
Tuwaheshimu Baba na Mama kwa matendo ya adabu, heshima, utii na mapendo (Ayu 3:12)
Twawakosea Heshima Baba na Mama kwa;
1. Tukiwakasirisha na kuwatukana
2. Tukiwakaidi na kuwapiga
3. Tukiacha kuwaombea
4. Tukiacha kuwasaidia katika shida na uzee. (Kut 21:15-17)
Wawalee hasa kwa mfano wao, kwa sala, kwa katekesi ya kifamilia na kushiriki maisha ya Kanisa
Tunakatazwa kuwatii watu wanaotuamuru jambo lililokatazwa na Mungu (Mdo 5:29)
Tumekatazwa haya;
1. Kukaidi wazazi na wakubwa wetu
2. Kuwakasirisha.
3. Kuwadharau.
Wakubwa hao ni;
1. Viongozi wa Kanisa
2. Viongozi wa Serikali
3. Walimu na walezi
4. Wakubwa wa kazi (War 13:1)
5. Viongozi wa Jumuiya
Updated at: 2024-05-27 06:44:47 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Updated at: 2024-07-16 11:49:22 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha kuwa tunaweza kuwaombea wafu ili wapate neema na amani ya Mungu? Ndio, Kanisa Katoliki linaamini kuwa tunaweza kuwaombea wafu ili wapate neema na amani ya Mungu. Imani hii imetokana na imani ya watakatifu wa kanisa na imani ya mapokeo ya kanisa kuhusu maombi kwa ajili ya wafu.
Kanisa Katoliki linatumia kifungu cha Waraka wa 2 Macabees 12:46 kuthibitisha kuwa tunaweza kuwaombea wafu. Katika kifungu hiki, inasimuliwa kuwa Judas Macabees aliwaombea wafu waliokuwa wamepoteza maisha yao vitani. Kanisa Katoliki linaamini kuwa maombi ya Judas yaliwasaidia wafu hao kupata nafuu na kumpendeza Mungu.
Pia, Kanisa Katoliki linatumia mfano wa Mtakatifu Paulo kufundisha juu ya umuhimu wa kutumia wakati wetu kuwaombea wafu. Katika Waraka wake kwa Timotheo, Paulo aliandika "Mimi nimekamilisha mbio, nimeumaliza mwendo, nimeilinda imani. Kuanzia sasa, taji ya haki imewekwa kando kwa ajili yangu, ambayo Bwana, hakimu mwenye haki, atanipa siku ile, wala si mimi peke yangu, bali na wote wao wanaopenda kufunuliwa kwake" (2 Timotheo 4:7-8). Paulo anahitimisha nafasi yake katika maisha na kuwa na uhakika wa kupokea taji ya haki. Kanisa linatumia mfano huu kuonyesha kuwa tunaweza kupokea taji ya haki kupitia maombi yetu kwa ajili ya wafu.
Kanisa Katoliki linatumia kifungu cha Kitabu cha Mithali 31:20 kufundisha juu ya umuhimu wa kuwaombea wafu. Kifungu hiki kinasema "Ananyosha mkono wake kwa wahitaji, ndiye anayewanyoshea watu wake mikono yake" na kanisa linatumia kifungu hiki kuonyesha kuwa tunahitaji kuwaombea wafu wetu ili waweze kupata amani na neema ya Mungu.
Kanisa Katoliki pia linasisitiza juu ya umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya kifo. Kanisa linaitwa kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya wafu, kama kupata Sakramenti ya Kitubio, kutolewa kwa Komunyo Takatifu na kutumia maombi maalum ya kwa ajili ya wafu. Kanisa linatufundisha kuwa, kwa kufanya hivyo, tunawasaidia wafu wetu kupata neema na amani ya Mungu katika maisha ya milele.
Kanisa Katoliki linatambua kuwa maombi kwa ajili ya wafu yanaweza kuwa na manufaa kwa wafu wenyewe, lakini pia kwa sisi waliobaki. Maombi haya yanaweza kutupa faraja na amani katika kipindi cha majonzi yetu. Kanisa linatuhimiza kwa maombi kwa ajili ya wafu wetu ili waweze kupata amani na neema ya Mungu.
Kwa kuhitimisha, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha kuwa tunaweza kuwaombea wafu ili wapate neema na amani ya Mungu. Imani hii inatokana na imani ya watakatifu na mapokeo ya kanisa. Kanisa linatumia Biblia na Catechism ya kanisa kuthibitisha umuhimu wa kuwaombea wafu. Kanisa linatuhimiza sisi sote kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya wafu na kuwaombea kupata amani na neema ya Mungu. Maombi kwa ajili ya wafu siyo tu kwa manufaa yao, lakini pia kwa ajili yetu waliobaki. Tuombe kwa ajili ya wafu wetu ili waweze kupata amani ya Mungu katika maisha ya milele. Amina.
Updated at: 2024-05-27 06:45:33 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Â
Â
Â
Â
Updated at: 2024-05-27 06:45:20 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Tumeamriwa tusadiki kuwa Mungu ni mmoja, ndiye Baba yetu na Mkubwa wetu: tumpende, tumwabudu yeye peke yake. (Mt 10:33, Kumb 6:4-9)
Tunamwabudu Mungu kwa sala , sadaka na matendo mema
Tumekatazwa kumdharau Mungu na kuweka imani yetu katika viumbe badala ya Mungu.
Ndiyo twamuheshimu Bikira Maria, Malaika na Watakatifu.
Kwa sababu hao ni washindi, rafiki wa Mungu na waombezi wetu.
Hatuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu tunawaheshimu tu.
Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22).
18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku. 20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. Kutoka 25 :18-22.
Vile vile Mungu alishawahi kuwaagiza Waisraeli Wachonge sanamu ya nyoka na yeyote atakayeumwa na nyoka akiiangalia atapona.
Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu.
Anayekosa kumuabudu Mungu ni yule;
1. Anayeacha kusali au anayesali hovyo
2. Anayemkufuru Mungu
3. Anayeamini na kushika mambo ya kipagani
Mambo hayo ni;
1. Kuabudu sanamu
2. Kufanya matambiko
3. Kwenda kwa waganga
4. Kupiga bao au ramli
5. Kuvaa hirizi
6. Kushiriki mambo ya kichawi n.k.
Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake.
Ni kuruhusu kitu chochote kimtawale mtu badala ya Mungu, mfano cheo, pombe, mali, shetani, tuisheni, kazi, na kutoadhimisha Jumapili au kutoshiriki.
Mkatoliki anaabudu kwa kupiga goti au magoti mawili na ni mbele ya sakramenti ya Ekaristi Takatifu tuu hasa wakati wa kuingia na kutoka kanisani
Magoti yanayopigwa wakati wa sala mfano kanisani, nyumbani, mbele ya sanamu, jumuiyani, shuleni yanaitwa Mkao wa sala
Tunaweka sanamu Kanisani kwa sababu tunaheshimu anayewakilishwa na sanamu hiyo kwa mfano Yesu Kristo, Mama Bikira Maria, Malaika na Watakatifu; na kamwe hatuziabudu. (Kutoka 25:18-22)
Hata Waisraeli kwenye hekalu lao walikua na sanamu kama tunavyosoma hapa;
"18 Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu; uyafanye ya kazi ya kufua, katika hiyo miisho ya kiti cha rehema, huku na huku. 19 Weka kerubi moja mwisho mmoja, na kerubi la pili mwisho wa pili; fanya hayo makerubi ya kitu kimoja na kiti cha rehema, mwisho huku na mwisho huku.20 Na hayo makerubi yatainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao, na nyuso zao zitaelekeana hili na hili; nyuso za hayo makerubi zitaelekea kiti cha rehema. 21 Weka kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha utie huo ushuhuda nitakaokupa ndani ya sanduku. 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :18-22.)"
Kwa hiyo kama Mungu mwenyewe aliagiza Sanamu za Malaika zichongwe na kusema atakua hapo na kuongea na watu wake. Je sio vyema zaidi kuwa na sanamu na Picha ya Mwanae wa Pekee Yesu Kristo na kuongea na Mungu mbele yake kama alitaka ya malaika ambao sio Mungu?
Mfano mwingine ni pale Mungu alivyomwabia Musa achonge Sanamu ya Nyoka wa shaba.
"BWANA akamwambia Mose, âTengeneza nyoka wa shaba na umweke juu ya mti, ye yote aliyeumwa na nyoka anaweza kumtazama na akaishi tena.ââ 9Kwa hiyo Mose akatengeneza nyoka wa shaba na kumweka juu ya mti. Kisha wakati mtu ye yote alipoumwa na nyoka, naye akamtazama yule nyoka wa shaba, aliishi."Â (Hesabu 21:8-9).
Kwa Mfano huu Je tunaweza kusema kuwa sanamu ya nyoka ina nguvu ya uponyaji kuliko ya Yesu aliye Mungu? Kumbuka hapa watu walioona sanamu hii ya nyoka hawakukoponywa na nguvu ya sanamu ya shaba bali kwa nguvu ya neema ya Mungu kupitia Imani kwa Mungu. Kwa hiyo unaposali mbele ya picha au sanamu hautegemei nguvu ya sanamu bali unategemea neema ya Mungu kwa njia ya Imani yako kwa Mungu.
Kama vile Sanamu hii ya nyoka aliyoagiza Mungu iwekwe ilivyowekwa kwa nia ya uponyaji kwa yule aitazamaye vivyo hivyo Sanamu na Picha za Kanisani zinawekwa kwa nia maalumu na kwa neema maalumu. Ndiyo maana hazifanani. Na zinabarikiwa kwa kuombewa Baraka Ili zizae neema kwa wanaozitumia.
Kuna tofauti kati ya kuabudu na kuheshimu. Wakatoliki wanaweka sanamu kwa heshima na sio kwa kuabudu, ndio maana unaposali mbele ya picha ya Yesu hausali ee sanamu nisaidie bali unasema ee Yesu nisaidie.
Je tuseme tunamwabudu Raisi kwa kuheshimu picha yake kwa kuiinamia? Je tunaabudu bendera kwa kuheshimu na kupigia saluti? Je taratibu zabunge za kutoa heshima na taratibu za mahakama ni kuabudu?. Je kuapa mbele ya picha ya Raisi ni kumuabudu Raisi? Je kuapa na Biblia ni kuabudu Biblia? Je tunapobusu Biblia na kuitunza kwa heshima tunaiabudu? Tofauti ya Biblia na sanamu ni nini? Je, kwenye Biblia kinachoheshimiwa ni karatasi au maana ya yale maneno kwenye karatasi. Pengine usingeheshimu kama hujajua kuyasoma.
Kuna tofauti gani kati ya biblia yenye Maandishi na msalaba wa kuchonga wenye kuonyesha kile kinachosemwa na biblia? kama unaweza kuheshimu biblia yenye karatasi tena pale unapoweza kuzisoma na pengine ungeizarau kama ni ya lugha tofauti na hujui kilichoandikwa? Je Msalaba uliobeba maana ya kile kilichoandikwa kwenye Biblia unaona si kitu? Kama Kinachoheshimiwa kwenye Biblia sio karatasi bali maana maneno yaliyoandikwa vivyo hivyo kinachoheshimiwa kwenye picha au sanamu sio chuma yake au mti ukiochongwa bali ni maana ya hiyo sanamu.
Hii ndio maana nasema kuna tofauti ya kuabudu na kuheshimu.
Kumbuka kuwa picha au sanamu yoyote ya Kikatoliki lazima ibarikiwe kwanza ndio uweze Kusali mbele yake. Inapobarikiwa inaombewa uwepo wa yule anayewakilishwa na picha/sanamu hiyo uwe pale sanamu ilipo na anayesali pale sala yake Ifike kwa mlengwa anayeonekana kwa ishara ya sanamu/picha. Kwa Mfano askofu au padri anapobariki sanamu ya Yesu anaomba kuwa "Yesu awepo pale kwenye sanamu na Neema zake", kwa hiyo yeyote anayesali mbele ya sanamu hiyo anaamini kuwa Yesu yuko pale na anasali Mbele yake. Kwa hiyo kinachopewa heshima sio ile sanamu bali ni yule anayeonekana kwa ishara ya ile sanamu au picha.
Daima Tumia Sanamu na Picha zilizobarikiwa kwani zimenuiwa uwepo wa yule inayemuwakilisha na utaongea naye hapo. Sisi tunaamini kwamba kwenye Sanamu ya Yesu kuna uwepo wa Yesu. Kama vile Mungu anavyowaambia Waisraeli katika (Kutoka 25 :22) baada ya kuwaagiza wachonge sanamu za Makerubi (Malaika) 22 Nami nitaonana nawe hapo, na kuzungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema, katikati ya hayo makerubi mawili yaliyo juu ya sanduku la ushuhuda, katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli. (Kutoka 25 :22). Sanamu au picha ni ishara wazi ya uwepo wa kile kisichoonekana.
Kwenye Agano la kale: Ndani ya hekalu la Waisraeli walikua na Sanduku la agano, sanduku hilo lilikua na vibao vya Amri za Mungu ambavyo ni Ishara ya Agano lao na Mungu na ndani ya sanduku kulikuwepo pia Mfano wa Kiti ambacho kimezugukwa na sanamu za viumbe kama malaika nyuso zao zikielekea kiti hicho Kutoka 25:10-22. Waisraeli walikua wanasali kuelekea sanduku la Agano wanapokuwa Hekaluni na hata wakiwa majumbani mwao walisali kuelekea upande lilipo Hekalu. Waisraeli walisali kuelekea Sanduku la Agano wakiamini kwamba Mungu yupo kati ya sanduku lile. Lakini sanduku lile halikuwa Mungu. Waisraeli waliona fahari juu ya Sanduku lile na walilithamini na kuliheshimu kwa kuwa lilionyesha uwepo wa Mungu na popote lilipokuwa waliamini Mungu yupo.
Kwenye Agano jipya:Â Wakristu wanasali Mbele ya Msalaba wa Yesu ambao unaonyesha kazi ya wokovu alioufanya Yesu kwa wanadamu ya Kuwakomboa watu kwa kifo chake Msalabani. Na Msalaba huo ni Ishara ya Ukombozi wa Agano jipya na la Milele. Kama ilivyokuwa kwa Sanduku la Agano, Wakristu wanaheshimu msalaba ambao ni ishara ya wokovu wao na wanaamini kuwa Mungu yupo kati ya Msalaba huo lakini Msalaba huo sio Mungu. Wakristu wanaona fahari juu ya msalaba wa Yesu kwa kuwa ndio ishara ya wokovu wao.
FUNZO:Kupitia Mfano wa Sanduku la Agano na Msalaba tunajifunza kuwa Vyote havikuwa Mungu ila vinaheshimiwa kwa Imani kuwa Mungu yupo pale. Vilevile, vyote ni ishara ya wazi ya Agano la Mungu na Wanadamu.
Tunasali mbela ya sanamu kwa sababu tunaamini sanamu inaakisi uwepo wa mhusika aliyechorwa au kuchongwa kwenye hiyo sanamu/picha. Ndio maana wakatoliki wanasali kwenye picha au sanamu iliyobarikiwa tuu kwa sababu Sanamu inapobarikiwa inaombewa uwepo wayule anayewakilishwa pale.
Tunafanya ishara ya msalaba kwenye sanamu kama sala ya utangulizi ambayo inathibitisha kuwa hatuabudu kile kilichoko pale bali kile tunachokifanya tunakifanya huku tukikiri Umungu na Heshima ya Utatu Mtakatifu (Mungu; Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.). Vile vile tunamtukuza Mungu katika Utatu Mtakatifu kwa sababu ya yule anayewakilishwa na picha au sanamu.
Hii ni ishara ya Upendo kwa yule anayewakilishwa kwenye picha au sanamu husika. Hata katika maisha ya kawaida watu hubusu picha za wazazi na wapendwa wao. Maana ni ile ile.
Tunawaheshimu kwa kuadhimisha sikukuu zao, kwa kuomba maombezi yao, kufuata mifano yao na kuheshimu masalia na sanamu zao, kwa kuinama kichwa kidogo tunapopita mbele yake
Updated at: 2024-05-27 06:45:19 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Updated at: 2024-07-16 11:49:15 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kanisa Katoliki limekuwa likitangaza utunzaji wa mazingira kama jukumu la kikristo kwa miaka mingi. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kwamba tunalinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo. Utunzaji wa mazingira ni kazi yetu sote na inatokana na imani yetu ya kikristo na maadili tunayoyafuata.
Katika kitabu cha mwanzo 2:15, Mungu anamwamuru Adamu awatunze na kuilinda bustani ya Edeni. Kwa hivyo, imani ya Kanisa Katoliki inaamini kwamba sisi ni wasimamizi wa mazingira na tunapaswa kulinda kila aina ya uhai uliopo. Kwa kufanya hivyo, tunawajibika kwa Mungu na kwa vizazi vijavyo.
Kanisa Katoliki linategemea falsafa ya kiekumene katika kutunza mazingira. Falsafa hii inasema kwamba binadamu na mazingira ni sehemu moja ya ulimwengu mmoja. Tunapata maisha yetu kutoka kwa mazingira na kwa hivyo, tunapaswa kuilinda mazingira kama sehemu ya jukumu letu la kibinadamu.
Vilevile, imeandikwa katika KKK 2402, "uharibifu wa mazingira ni kinyume cha maadili na inaweza kuathiri maisha ya watu." Kwa hivyo, Kanisa linasisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kama sehemu ya maadili yetu.
Katika Mkutano wa Mazingira wa Vatican uliofanyika mnamo 2019, Baba Mtakatifu Francis aliwataka watu wote kuchukua hatua za kuhifadhi mazingira. Aliwataka wakristo kuhakikisha kwamba wanawajibika kwa kufuata mafundisho ya kanisa na kuishi maisha yenye kuheshimu mazingira.
Kwa hivyo, tunapaswa kulinda mazingira kwa kufuata kanuni za utunzaji wa mazingira kama vile kupunguza utumiaji wa plastiki na kukuza utumiaji wa nishati mbadala. Tunapaswa pia kuhakikisha kwamba tunatumia rasilimali za dunia kwa njia yenye uwajibikaji na kwa kuzingatia mahitaji ya vizazi vijavyo.
Kwa kuhitimisha, Kanisa Katoliki linatukumbusha kwamba utunzaji wa mazingira ni jukumu letu kama wakristo. Tunapaswa kuhakikisha kwamba tunatumia rasilimali za dunia kwa njia yenye uwajibikaji na kuheshimu kila aina ya uhai uliopo. Tunapaswa kuwa wasimamizi wa mazingira na kutoa mfano wa maisha yenye kuheshimu mazingira kwa vizazi vijavyo.
Updated at: 2024-05-27 06:44:57 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Updated at: 2024-05-27 06:45:37 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)