Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu matakwa ya Mungu na mapenzi ya binadamu?
Welcome Back.
Updated at: 2024-07-16 11:49:13 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Kanisa Katoliki linatambua kuwa Mungu aliumba ulimwengu na binadamu kwa mapenzi yake, lakini pia Mungu alitupa uhuru wa kuchagua. Ni wajibu wa binadamu kutimiza matakwa ya Mungu na kuishi maisha yanayoambatana na mapenzi yake.
Katika Waraka wa Yohane Paulo II, Fides et Ratio, Kanisa Katoliki linatilia mkazo kwamba binadamu ana jukumu la kutafuta ukweli na kuelewa mapenzi ya Mungu. Kupitia kwa imani na akili, binadamu anaweza kufikia maarifa ya ukweli huu.
Katika Maandiko Matakatifu, tunaona jinsi ambavyo Mungu anatutaka kufuata mapenzi yake. Mtume Paulo aliandika katika Waraka wa Waebrania 10:36, "Kwa hiyo, ninyi mnahitaji subira ili mtimize mapenzi ya Mungu na mpokee ahadi yake." Hii inamaanisha kuwa kwa kumtii Mungu na kufuata mapenzi yake, tunaweza kufikia ahadi zake.
Kanisa Katoliki linamfundisha mtu anapaswa kumtii Mungu na kusubiri mapenzi yake. Hii inamaanisha kuwa tunapaswa kufuata amri za Mungu na kuishi maisha yenye haki na kwa upendo. Katika KKK 2822, inasemekana, "Tunatafuta mapenzi ya Mungu katika maisha yote, hasa katika maamuzi yetu muhimu."
Katika Maandiko Matakatifu, tunajifunza kwamba Mungu anataka tufanye kazi yetu kwa bidii na kwa upendo. Paulo aliandika katika Waraka wa Wakolosai 3:23-24, "Kila mfanyalo, fanyeni kwa moyo wenu wote, kama kwa Bwana, si kwa ajili ya wanadamu, kwa maana mnajua ya kuwa mtapokea ujira wa mrithi kutoka kwa Bwana."
Kanisa Katoliki linatilia mkazo kwamba inatupasa kufanya kazi kwa heshima na kwa uaminifu, kwa kuwa kwa kufanya hivyo tunamfurahisha Mungu. Kanuni ya Maadili ya Kikatoliki inatufundisha kuwa tunapaswa kutoa kazi yetu kwa Mungu na kuifanya kwa uangalifu na upendo, ili kuonyesha upendo wetu kwa Mungu.
Kwa hiyo, Kanisa Katoliki linatambua kwamba tunapaswa kutimiza matakwa ya Mungu na kuishi maisha yanayoambatana na mapenzi yake. Tunapaswa kumtii Mungu, kufanya kazi yetu kwa bidii na kwa upendo, na kutafuta ukweli na maarifa ya mapenzi yake. Kwa kufanya hivyo, tunapata baraka za Mungu na kupokea ujira wake wa milele.
Miaka zaidi ya 3000 iliyopita katika mji wa Yeriko alikuwepo mwanamke mmoja kahaba, jina lake Rahabu. Huyu mwanamke aliwaokoa wapelelezi wa Israel waliotumwa kwenda kufanya uchunguzi ktk nchi yao.
Wakati wana wa Israel wanatoka Misri kuelekea nchi ya Kaanani, Mungu aliwaahidi kuwapa mji wa Yeriko. Kwahiyo walipofika ng'ambo ya mto Yordani, Yoshua akatuma wapelezi wawili kwenda kuipeleleza Yeriko kabla wana wa Israel kuivamia na kuitwaa.
Updated at: 2024-07-16 11:49:43 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Miaka zaidi ya 3000 iliyopita katika mji wa Yeriko alikuwepo mwanamke mmoja kahaba, jina lake Rahabu. Huyu mwanamke aliwaokoa wapelelezi wa Israel waliotumwa kwenda kufanya uchunguzi ktk nchi yao.
Wakati wana wa Israel wanatoka Misri kuelekea nchi ya Kaanani, Mungu aliwaahidi kuwapa mji wa Yeriko. Kwahiyo walipofika ng'ambo ya mto Yordani, Yoshua akatuma wapelezi wawili kwenda kuipeleleza Yeriko kabla wana wa Israel kuivamia na kuitwaa. Wale wapelelezi walipofika mji wa Yeriko mfalme akapelekewa taarifa kuwa kuna watu wawili wameingia kuipeleleza nchi.
Kwahiyo mfalme akaagiza wakamatwe na wauawe. Wale wapelelezi wakaingia ktk nyumba ya mwanamke kahaba aitwaye Rahabu akawaficha darini. Akawafunika kwa mabua ya kitani. Wale askari walipofika na kumuuliza Rahabu kwamba wako wapi waisrael wawili walioingia humu ndani, Rahabu akajibu kuwa wameondoka.
Akasema ni kweli waliingia ktk nyumba yangu lakini walitoka kabla lango la mji halijafungwa. Akawaambia wafuateni haraka kabla hawajafika mbali. Wale askari wakatoka kuwafuata wale wapelelezi hadi katika vilima vya nje ya mji lakini wasiwaone. Ilipofika usiku Rahabu akawashusha darini wale wapelelezi na kuwaelekeza namna ya kutoroka mji wa Yeriko. Akawaelekeza wapite njia nyingine tofauti na ile waliyoiendea wale askari. Akawashusha kupitia dirishani ili watu wa mji ule wasiwaone.
Kwa ukarimu aliowatendea wale wapelelezi wakaweka agano nae kwamba siku wana wa Israel wakija kuiangamiza Yeriko, BWANA ataiponya nyumba ya Rahabu na ndugu zake wote. Ili kutimiza agano hilo wale wapelezi wakamwambia Rahabu weka kamba nyekundu katika dirisha lako kama alama, ili jeshi la Israel liltakapouteketeza mji nyumba yako isiangamizwe.
Yoshua 2:17 &18 "Wale wapelelezi wakamwambia Rahabu, Sisi tunataka tusiwe na hatia kwa ajili ya kiapo hiki ulichotuapisha. Angalia, tutakapoingia katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu katika dirisha hili ulilotuteremshia; nawe uwakusanye nyumbani mwako, baba yako, mama yako, na ndugu zako, na watu wote wa nyumba ya baba yako."
Rahabu akafanya hivyo, na siku Jeshi la Israel lilipovamia Mji wa Yeriko ili kuuteketeza, Rahabu na ndugu zake walipona.
Yoshua 6:23 &24 "Basi wale vijana wapelelezi wakaingia, wakamtoa Rahabu, na baba yake, na mama yake, na ndugu zake, na vitu vyote walivyokuwa navyo, wakawatoa na jamaa zake wote pia; wakawaweka nje ya matuo ya Israeli. Kisha wakauteketeza mji kwa moto, na vitu vyote vilivyokuwa ndani yake…"
MORAL OF THE STORY.!
Habari hii ina mengi ya kutufundisha lakini leo nataka nikufundishe kuhusiana na siri ya kamba nyekundu ambayo Rahabu aliiweka katika dirisha lake na jinsi ilivyomuokoa.
Rahabu hakua mtakatifu, hakuwa mteule wa Mungu wala hakuwa kizazi cha Israel. Alikua mwanamke wa mataifa, tena kahaba. Hakuwa mwema sana machoni pa Mungu. Lakini aliokoka kwa sababu ya "kamba nyekundu" dirishani mwake. Pengine wapo maaskofu, wachungaji, mitume au manabii walioangamizwa, lakini kahaba Rahabu akaokolewa yeye na ndugu zake licha ya kwamba alikua kahaba. Siri ni "kamba nyekundu" dirishani mwake.
Jiulize je wewe unayo kamba nyekundu? Kuna watu katika maisha wanaonekana wenye dhambi, wachafu, dhaifu au wasiofaa, lakini Mungu huwanyanyua na kuwabariki na kuwaacha wale tunaodhani ni watakatifu au wenye haki. Mungu anaangalia "kamba nyekundu". Unaweza kuwa mtakatifu lakini huna "kamba nyekundu" itakayomfanya Mungu akurehemu.
Unaweza kuwa umemaliza masomo yako na umefaulu vizuri, lakini kila unapoomba kazi huitwi hata kwenye usaili, na ukiitwa hupati kazi, miaka inazidi kwenda. Unaamua kwenda kwenye maombi. Kila siku unafanya maombi lakini bado hufanikiwi. Unajiuliza tatizo liko wapi. Unaji-asses na kuona hakuna tatizo mahali. Kumbe huna "kamba nyekundu"
Au unaweza kuwa una biashara yako lakini haifanikiwi. Hupati wateja. Umehitahidi kwa kila hali lakini bado huoni faida. Unadhani tatizo labda Mungu amekuacha. Unaamua kuwa mtu wa maombi. Unazunguka makanisa mbalimbali kuonbewa lakini bado haufanikiwi. Kumbe huna "kamba nyekundu".
"Kamba nyekundu" imekuwa siri ya mafanikio ya watu wengi bila kujalisha mahusiano yao kiroho na Mungu. Bila kujalisha kama ni wakristo au si wakristo. Kamba nyekundu imewasaidia hata wenye dhambi kubarikiwa. Rahabu alikua kahaba lakini yeye na ndugu zake waliokolewa kwa sababu ya "kamba nyekundu".
Je kamba nyekundu ni nini? Kamba nyekundu ni mfumo wako wa maisha; jinsi unavyoishi na unayowatendea watu wengine, hasa "wateule" wa Mungu.
Kuna wakati Mungu huamua kukubariki si kwa sababu wewe ni mwema sana, bali kwa sababu kuna watu wema wanaoomba kwa ajili yako. Inawezekana tangu uanze kuomba, maombi yako hayajawahi kufika kwa Mungu lakini unabarikiwa, kwa sababu ya kamba nyekundu.
Kuna watu ambao ni "wateule" wa Mungu, kwahiyo kadri unavyowatendea mema hao watu baraka zinakuja kwako "automatically" hata kama wewe si mkristo. Rahabu aliwatendendea mema wapelelezi wa Israel baraka zikaenda kwake "automatically" bila kujalisha kwamba alikua kahaba.
Yatima, wajane, maskini, wazee, wagonjwa na wengine wenye uhitaji ni wateule wa Mungu. Kwahiyo ukiwatendea mema watu hawa baraka zinakuja kwako hata kama wewe ni mwenye dhambi.
Kwa mfano kama kuna watoto yatima unawasomesha, au kuna wajane unawasaidia mahitaji yao, au wagonjwa unawasaidia matibabu, si rahisi Mungu kuondoa mkono wake wa baraka kwako hata kama wewe ni mwenye dhambi. Mungu akiondoa baraka kwako watu wake watateseka.
Wale yatima, wajane, wagonjwa ambao wewe ni msaada kwao kila wakiomba Mungu huongeza baraka kwako ili uzidi kuwahudumia. Inawezekana maombi yako hayafikagi kwa Mungu lakini unabarikiwa kwa sababu ya maombi ya hao unawaosaidia.
Kuna wakati Mungu anaweza kuamua kuzipiga dhoruba biashara za wenzako, lakini ya kwako ikasimama imara. Si kwa sababu wewe ni mwema sana, bali kwa sababu kuna watu wanamlilia Mungu kwa ajili yako. Kuna wanategemea ada za shule kwenye hiyo biashara yako. Kuna watu wanategemea pesa za matibabu kwenye biashara yako. Kwa hiyo Mungu akiyumbisha biashara yako atakua anawaumiza watu hao. So ili asiwaumize anaamua kukuaacha. Hiyo ni kamba nyekundu.!
Kuna wakati wenzio wakifanya makosa madogo kazini wanafukuzwa kazi, lakini unajishangaa wewe umefanya makosa makubwa na hufukuzwi. Si kwa sababu una bahati sana. Ni kamba nyekundu. Kuna watu walioko nyuma yako ambao ni wateule wa Mungu. Kuna yatima wanategemea kulipiwa ada kwa mshahara wako, kuna wagonjwa wanategemea kusaidiwa hela za matibabu kwenye mshahara wako, kuna wajane wanategemea hela ya kuishi kutoka kwako. Kwahiyo Mungu akikuadhibu anakua amewaadhibu na wao. Kwahiyo ili wapone inabidi akulinde hata kama umefanya kosa kazini. Unashangaa tu kesi imeisha hata kwa namna ambayo hujui. Hiyo ni kamba nyekundu.!
Kuna mtu ambaye ni maskini wa kutupwa hana hata uwezo wa kununua sukari. Lakini anamuomba Mungu kwa imani kuwa ampe sukari aweze kunywa chai kila siku. Kwa kuwa huyo maskini huwa anapata sukari kutoka kwako, Mungu atazidi kukubariki ili uendelee kumhudumia huyo maskini. Hiyo ni Kamba nyekundu.!
Kamba nyekundu ilimuokoa Rahabu na ndugu zake licha ya kwamba alikua kahaba. Jiulize wewe una kamba nyekundu? Je kuna watu wako nyuma yako ambao Mungu akiwaangalia anakubariki, anakuokoa hata kama upo kwenye hatari?
Kama unamsomesha mwanao shule ya "mamilioni" kwa mwaka wakati mtoto wa jirani yako hana hata uniform za kuendea shule, au unatumia "mamilioni" kwa pombe na starehe wakati kuna wagonjwa wanaokufa kwa kukosa panadol, siku Mungu akitaka kukuadhibu hajiulizi mara mbili maana huna "kamba nyekundu" nyuma yako.
Lakini yule anayesaidia wenye uhitaji, kama yatima, wagonjwa, wazee, wajane,walemavu, au maskini atazidi kubarikiwa tu hata kama ni mwenye dhambi, maana anayo kamba nyekundu.
Hii ni kwa sababu Mungu akitaka kumuadhibu, kabla hajamtizama yeye anatizama kwanza yatima walioko nyuma yake anaowasaidia, anatizama wagonjwa wanaomtegemea kwa matibabu, anatizama wajane. Anaona akimuadhibu, atakuwa ameadhibu na hao wanaomtegemea. Kwa hiyo anaamua kumuacha.
Hii ina maana kuwa baraka na utakatifu ni vitu viwili tofauti. Unaweza usiwe mtakatifu lakini Mungu akakubariki na akakulinda. Unaweza kubarikiwa si kwa sababu unastahili, bali kwa sababu kuna "wanaostahili" wapo nyuma yako wakikupigania kwa baba yao (Yehova). Ndio maana kuna watu wengi wasio Wakristo wanabarikiwa kila siku hata kama hawamjui Mungu. Ni kwa sababu wana "kamba nyekundu".
Malisa G.J
Updated at: 2024-07-16 11:49:36 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na Papa wa Roma ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Hakuna uamuzi wa kudumu kuhusu ipi ni mikuu kati ya mitaguso yote iliyofanyika katika historia ya Kanisa. Tangu karne XVI Wakatoliki wataalamu wa sheria za Kanisa wanatoa orodha yao, ambayo kwa sasa ni kama ifuatavyo.
ORODHA YA MITAGUSO MIKUU
• Katika milenia ya kwanza ilifanyika mashariki (Uturuki wa leo):
1. Nisea I (mwaka 325)
2. Kostantinopoli I (381)
3. Efeso (431)
4. Kalsedonia (451)
5. Kostantinopoli II (553)
6. Kostantinopoli III (680-681)
7. Nisea II (787)
8. Kostantinopoli IV (869-870)• Katika milenia ya pili ilifanyika magharibi (Italia, Ufaransa, Ujerumani, Uswisi na Vatikano ya leo):
9. Laterano I (1123)
10. Laterano II (1139)
11. Laterano III (1179)
12. Laterano IV (1215)
13. Lyon I (1245)
14. Lyon II (1274)
15. Vienne (1311-1312)
16. Konstanz (1414-1418)
17. Firenze (1431-1445)
18. Laterano V (1512-1517)
19. Trento (1545-1563)
20. Vatikano I (1869-1870)
21. Vatikano II (1962-1965)
Updated at: 2024-07-16 11:49:09 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Huruma ya Mungu: Faraja katika Majaribu na Huzuni
Katika maisha, tunakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinatulemea na kutufanya tujisikie kutokuwa na nguvu. Hali hii inaweza kusababisha majaribu na huzuni. Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo kwa watoto wake. Huruma ya Mungu ni faraja kubwa katika kipindi cha majaribu na huzuni.
Huruma ya Mungu inatufariji Mungu anaahidi kutufariji katika kipindi cha majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika Zaburi 34:18, "Bwana yu karibu na wale waliovunjika moyo, huwaokoa waliopondeka roho." Mungu anatufariji kwa kutoa faraja ya kweli na upendo wake usio na kikomo.
Huruma ya Mungu inatuponya Huruma ya Mungu inaweza kutuponya kutokana na majeraha ya kihisia na kimwili. Kama ilivyoandikwa katika Isaya 53:5, "Lakini yeye alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona." Mungu anaweza kutuponya kutokana na majeraha yoyote tunayopitia.
Huruma ya Mungu inatupatia nguvu Mungu anatupa nguvu ya kuvumilia wakati wa majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika 2 Wakorintho 12:9, "Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; kwa kuwa nguvu yangu hutimilika katika udhaifu." Tunaweza kupata nguvu yetu kutoka kwa Mungu.
Huruma ya Mungu inatupa matumaini Mungu anatupa matumaini katika kipindi cha majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika Warumi 15:13, "Mungu wa matumaini na awajaze furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kuzidi kwa nguvu ya Roho Mtakatifu." Tunaweza kuwa na matumaini kwa sababu ya upendo na huruma ya Mungu.
Huruma ya Mungu inatupa msamaha Mungu anatupa msamaha kwa dhambi zetu na kutusamehe wakati wa majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika Zaburi 130:3-4, "Ikiwa wewe, Bwana, utakumbuka maasi, Ee Bwana, ni nani atakayesimama? Bali kwako kuna msamaha, Ili uogopwe." Tunaweza kupata msamaha wa Mungu kwa kuomba na kutubu.
Huruma ya Mungu inatupatia upendo Mungu anatupatia upendo wa kweli katika kipindi cha majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika 1 Yohana 4:16, "Nasi tumejua na kusadiki upendo ule ambao Mungu anao kwetu. Mungu ni upendo, naye akaaye katika upendo akaa ndani ya Mungu, na Mungu akaa ndani yake." Tunaweza kupata upendo wa Mungu kwa kuwa na uhusiano wa karibu naye.
Huruma ya Mungu inatupa uvumilivu Huruma ya Mungu inaweza kutupa uvumilivu wakati wa majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika Yakobo 1:2-4, "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu mnapoangukia katika majaribu mbalimbali, mkijua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Lakini saburi na iwe na kazi kamili, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu pasipo na kasoro yo yote." Tunaweza kuwa na uvumilivu kwa sababu ya huruma ya Mungu.
Huruma ya Mungu inatupa imani Mungu anatupa imani katika kipindi cha majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika Waebrania 11:1, "Basi, imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana." Tunaweza kuwa na imani kwa sababu ya Mungu anayetuaminisha.
Huruma ya Mungu inatupa uzima wa milele Mungu anatupa uzima wa milele katika kipindi cha majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika Yohana 3:16, "Kwa kuwa jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Tunaweza kuwa na uhakika wa uzima wa milele kupitia kwa imani yetu kwa Mungu.
Huruma ya Mungu inatupa sababu ya kufurahi Mungu anatupa sababu za kufurahi hata wakati wa majaribu na huzuni. Kama ilivyoandikwa katika Wafilipi 4:4, "Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini." Tunaweza kufurahi kwa sababu ya upendo na huruma ya Mungu kwetu.
Katika Katekisimu ya Kanisa Katoliki, tunakumbushwa juu ya huruma ya Mungu kama "kazi ya pekee ya Mungu ambayo inashinda kila kitu, inaonyesha uweza wake wa kupenda zaidi kuliko kuteseka, uweza wake wa kuwa mwenye upendo kuliko yote" (CCC 182). Katika "Diary of Saint Maria Faustina Kowalska," tunasoma juu ya huruma ya Mungu kwa mwanadamu: "Nimepata utulivu wa nafsi katika juhudi ya kuwa karibu na Mungu, katika huruma yake na katika kuwa na imani kwake" (D 85).
Watakatifu wa Kanisa Katoliki kama Teresa wa Avila na Francis wa Assisi wametambua huruma ya Mungu katika maisha yao na wamewahimiza wengine kutafuta huruma hiyo. Kwa kweli, huruma ya Mungu ni faraja kubwa katika kipindi cha majaribu na huzuni. Tunaweza kumgeukia Mungu kwa imani na tumaini katika kipindi hiki na kujua kwamba yeye daima yuko upande wetu. Je, wewe umepata faraja ya huruma ya Mungu katika maisha yako?
Updated at: 2024-07-16 11:49:32 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
➡ Asubuhi saa 12 : 00 mtu anaamka, kabla hata HAJAMUSHUKURU MUNGU, kabla hata hajatoka kitandani, kabla hata hajajifunua shuka,
👉ATARIPOTI KWA SIMU KWANZA KABLA YA KURIPOTI KWA YEYOTE, NDIO HAPO UNAONA MTU AKIAMKA KABLA HATA HAJASALI KWA MUNGU ANAAMKIA SIMU KWANZA KUIKAGUA,
- Nani alinitafuta?
-Nani alini-text?
-WhatsApp nani kanitumia msg?
- kwenye magroup kuna mpya gani?
- Fb kuna post gani kali?
- nani kaweka picha kali leo?
Updated at: 2024-07-16 11:49:45 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
➡ Asubuhi saa 12 : 00 mtu anaamka, kabla hata HAJAMUSHUKURU MUNGU, kabla hata hajatoka kitandani, kabla hata hajajifunua shuka,
👉ATARIPOTI KWA SIMU KWANZA KABLA YA KURIPOTI KWA YEYOTE, NDIO HAPO UNAONA MTU AKIAMKA KABLA HATA HAJASALI KWA MUNGU ANAAMKIA SIMU KWANZA KUIKAGUA,
- Nani alinitafuta?
-Nani alini-text?
-WhatsApp nani kanitumia msg?
- kwenye magroup kuna mpya gani?
- Fb kuna post gani kali?
- nani kaweka picha kali leo?
Nk.
Akimaliza KURIPOTI KWA Simu, faster faster, anapiga kaombi ka kidesturi, sekunde 20 basi.
Biblia ipo hapo kando tu ya kitanda, lkn anaona hana muda wa kuisoma.
✴BADALA YA KUANZA SIKU NA BWANA, MTU ANAANZA SIKU NA SIMU.
Pamoja na kazi za kuutwa, za mtu huyo, lkn atafanyq juu chini, apate muda wa KURIPOTI kwa SIMU.
Lakini mtu huyo huyo, hawez kbsa kupata muda wa kujitenga angalau kwa dk 3 tu, kw kutwa nzima ARIPOTI KWA MUNGU KWA NJIA YA MAOMBI.
Ana muda wa kusoma status kwenye social media kutwa nzima,
Lkn hana muda kbsa wa kupitia angalau sura moja tu, ya Biblia kwa siku.
Ana bundle la dk, sms, WhatsApp kila siku, lkn hana sadaka ya kumtolea Mungu.
Umeme ukikatika kutwa moja tu, akakosa kuwa na simu sababu ya chaji, anajisikia mpwekee, siku anaiona ndefuu, anajiona amepungukiwa saana!
Lakini huyo huyo, siku nzima inaisha, na ya pili, ya tatu , hajawahi kuwa na muda na Mungu wake hata kidogo, na anaona ni sawa tu.
Hata ktk siku ya ibada, yale masaa machache tu ya ibada, ambapo inatakiwa iwe ni mtu na Mungu wake tu, bila kuingiliwa na chochote, 👉mtu bado hawezi kukaa bila KURIPOTI kwa simu, ibada inaendelea huku mtu kawasha data, na anasoma na kujibu msg zake km kawaida.
👉 au kama ana kaustaraabu kidogo, atatoka nje, huko anaenda kukagua msg, kuangalia updates nk.
SIMU UNAYO KUTWA, KUCHWA, KIIILA SIKU, YANI HUKUWEZA KUVUMILIA KUIWEKA PEMBENI KWA MASAA TU?
➡ Swali nauliza, Mtu wa aina hiyo Mungu wake ni nani?
" Usiwe na miungu mingine ila mimi".
KUTOKA 20 : 3
Kumuabudu Mungu peke yake, ni kumfanya Mungu awe wa KWANZA MOYONI NA MAWAZONI MWAKO.
Kumfanya awe kipaumbele kwenye kiila ulitendalo.
➡WENGI WAMEZIFANYA SIMU ZAO, ZICHUKUE NAFASI YA MUNGU KATIKA MIOYO, FIKRA NA MAISHA YAO KWA UJUMLA.
➡Wamekuwa tayari kupoteza karibu kiila kitu kwa ajili ya simu
- kupoteza marafiki > hawana muda na marafiki zao, wanajifungia ndani, wakichati.
- hawana muda na wazazi wao, hata kama wanaishi nyumba moja. > kijana akifika nyumbani, anapitiliza chumbani, ni yeye na simu, ataonekana muda wa kula tu, tena sometimes hata mezani anakuwa na simu, pale mezani wako wazazi wake kbsa, ndugu zake nk, lkn hajali uwepo wao, anaendelea na simu tu.
- Hawana muda na Mungu > Anahakikisha vyovyote itakavyokuwa, muda wa kuwa na simu unapatikana, HATA KAMA HILO LITAMAANISHA KUUPORA MUDA WA MUNGU (muda wa ibada).
Atakosa fedha za kusaidia wahitaji, fedha za zaka na sadaka, lkn fedha ya SIMU, (bundles) , lzm inakuwepo.
➡Mtu wa aina hiyo, anaiabudu simu bila kujua.
➡KITU CHOCHOTE KINACHOUVUTA MOYO KUTOKA KWA MUNGU, KUKIELEKEA CHENYEWE, KITU HICHO KINAJARIBU KUCHUKUA NAFASI YA MUNGU MOYONI.
NB: Sio lengo langu kupinga matumizi ya simu, lkn nilitaka tuwe na kiasi.
Updated at: 2024-07-16 11:49:35 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Biblia inashuhudia kuwa watu wanatofautiana
Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na jinsi walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili ya taifa lake.Abrahamu alimuamini Mungu akawa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18).Yosefu, mwana mpenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20).Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale: aliongoza Israeli kutoka [[utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya Agano la Kale yanakiri, “Wala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musa” (Kumb 34:10-12).Waliofuata ni Yoshua, Debora, Gideoni, Ruthu, Samweli, wafalme Daudi na Solomoni, manabii Eliya, Isaya, Yeremia, Ezekieli na wengineo.Mwishoni Yesu Kristo akamsifu Yohane Mbatizaji akisema, “Ni mkuu kati ya uzao wa wanawake” (Lk 7:24-28).Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, “Mama wa Bwana wangu” (Lk 1:43).Bikira Maria si mtu wa ziada katika mpango wa Mungu bali ni mshiriki mkuu wa ukombozi wa binadamu. Maria amechangia wokovu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa. Msimamo wake ulikuwa mmoja tu: “Tazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk 1:38).Tukichunguza nafasi yake katika fumbo hilo, tunaweza kukiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49), kwa kuwa, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27).Yale yote ambayo Wakristo wengi wanayasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia bali alijaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiitikia kwa hiari fumbo la mpango wake.
Utabiri kuhusu Bikira Maria kwenye Biblia
Biblia inatupatia utabiri uliotolewa na Mungu mwanzoni mwa historia kuhusu mwanamke atakayemshinda nyoka wa kale (Shetani): “Nitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chako” (Mwa 3:15). Juu ya [[Eva wa kale, ambaye alidanganywa na kuangushwa na Shetani atende dhambi, imesemwa: “Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio hai” (Mwa 3:20). Hata hivyo Adamu na Eva wa kale wametuletea kifo (Rom 5:12). Mababu wa Kanisa wanamtazama Bikira Maria kama Eva mpya aliyemshinda Ibilisi na kuwa mama wa wote walio hai. Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Mama yake awe Mama wa waliokombolewa kwa kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. “Penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Kleopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, “Mama, tazama, mwanao”. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, “Tazama, mama yako”. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. (Yoh 19:26-27).Utabiri mwingine ulisema, “Tazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi” (Isa 7:14). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:34-35, “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”. “Imba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yako” (Sef 3:14-15). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:28: “Malaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, ‘Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja nawe’”. “Umebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika. Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu milele” (Yudithi 14:7; 15:9). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:42, “Akapaza sauti kwa nguvu akasema, ‘Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwa’”.Bikira Maria ni fumbo la ajabu alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Jamaa yake Elizabeti alimpongeza tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, “Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwana” (Lk 1:45).Hivyo manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua Maria kwa heshima. Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yalitimia katika Agano Jipya: ukombozi ulianza Bikira Maria alipokubali kwa imani fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu. Bikira Maria hakuwa “chombo” tu kilichotumika bila ya kuelewa, bali alikuwa mshiriki huru wa kazi ya ukombozi ya Mwanae, kwa kuwa alipopashwa habari na malaika alikubali kwa hiari mpango wa Mungu akisema, “Mimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonena” (Lk 1:38).
Bikira Maria katika maisha ya Yesu
Yesu, kama mtu yeyote mcha Mungu, aliwaheshimu na kuwatii wazee wake: “Basi, akarudi pamoja nao Nazareti, akawa anawatii” (Lk 2:51).Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara ya Yesu iliongozwa na Bikira Maria katika arusi ya Kana ya Galilaya, akisukumwa na huruma kwa wenye shida: kwa ombi lake Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake wakamwamini. Yohane alisimulia hivi, “Siku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, ‘Hawana divai’. Yesu akamwambia, ‘Mama tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia’. Mamaye akawaambia watumishi, ‘Lo lote atakalowaambia, fanyeni’. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, ‘Jalizeni mabalasi maji’. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, ‘Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza’. Wakapelekea. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maj), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, ‘Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa’. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. (Yoh 2:1-12).Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake kuu kabisa, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya roho kuliko ya mwili. “Basi, mtu mmoja akamwambia, ‘Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema nawe’. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, ‘Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?’ Kisha akanyosha mkono wake juu ya wanafunzi wake akasema, ‘Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na mama yangu’” (Math 12:46-50). Vilevile, wakati wa utume wake, alimsikia “mwanamke mmoja katika lile kundi la watu akisema, ‘Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha’. Yesu akamjibu, ‘Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na kulishika’” (Mk 11:27-28).
Bikira Maria alivyoshiriki Mateso ya Yesu
Katika kumfuata Mwanae Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni uchungu kama upanga utakaopenya moyo wake, “Tazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama upanga utauchoma moyo wako” (Lk 2:34-35).Bikira Maria alishiriki kwanza mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiuawe na Herode Mkuu, “Hivyo Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka Herode alipokufa” (Math 2:14-15).Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua kuteswa kwa Yesu; wanafunzi walipokimbia au kumtazama kwa mbali, yeye alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata Mwanae. Kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, alipoyashuhudia yote aliteseka sana katika moyo wake safi, kiasi kwamba Bernardo wa Klervoo akasema, “Msalaba wa Yesu uliwasulubisha wote wawili, Yesu mwilini na Mama yake moyoni”. Uaguzi wa mzee Simeoni ulitimia hivyo.Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, “Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo” (Kol 1:24). “… maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake” (Rom 8:17b).Pale msalabani Bikira Maria, kwa njia ya mtume Yohane alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae; kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana ameshindwa.
Bikira Maria baada ya kifo cha Yesu
Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, akilivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa sala yake. “Hao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na ndugu zake” (Mdo 1:14).Yesu alisema, “Ninayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa kadiri ya utabiri wake kuwa ataheshimiwa na vizazi vyote, “Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote wataniita mwenye heri” (Lk 1:48).
Watu wawili👬 walikuwa wanakunywa pombe🍺🍻 baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana🙅🏾♂ na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi.
Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga. Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena.
Kumbe amemwua mwenzie.😰
Updated at: 2024-07-16 11:49:44 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Watu wawili👬 walikuwa wanakunywa pombe🍺🍻 baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana🙅🏾♂ na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi.
Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga. Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena.
Kumbe amemwua mwenzie.😰
Ndipo alipoanza kukimbia🏃🏾 huku shati laki likiwa limechafuka sana na damu. Wale waliyokuwa wanauangalia ule ugomvi wakaanza kumfukuza.
🏃🏾 🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾
Huyu mwuaji akakimbilia kwenye 🏡🏃🏾nyumba ya mtu mmoja mcha Mungu na akamwomba yule mtu amfiche maana ameua mtu na watu walikuwa wanamfukuza.
Yule mcha Mungu akasema nitakuficha wapi wakati mimi nina chumba kimoja tu?😨
Yule mwuaji akamjibu akamwambia acha kuendelea kupoteza wakati fikiria tu mahali pa kunificha. Yule mcha Mungu akavua shati👔 lake safi akampa yule mwuaji alafu yeye akachukua lile shati la muaji lililojaa damu akalivaa.
Akampa sharti yule mwuaji na kumwambia tunza shati langu usilichafue. Yule mcha Mungu alipofungua mlango wa chumba chake wale watu wakamvamia🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾🏃🏿♀🏃🏾 na kumpiga sana wakijua yeye ndo mwuaji huku mwuaji akiondoka salama na kurudi kwake.
Baada ya kumpiga sana yule ndugu akapelekwa polisi👮🏾👮🏽♀ na baadaye akapelekwa mahakamani na akahukumiwa kunyongwa👴🏼 kwa kumwua mtu mwingine.
Yule mwuaji halisi akiwa kule nyumbani alijisikia vibaya sana😞 akaenda mahakamani akajisalimisha akasema yeye ndiye aliyeua, yule ndugu aachiwe huru.
Hakimu⚖ akamwambia umechelewa, yule ndugu kesha nyongwa.
Alilia😭😩 sana na kujiambia kuwa yule mtu amekufa kwa kosa ambalo sio lake.😰
Akakumbuka maneno ya mwisho ya yule ndugu _*"LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE."*_
Wapendwa,
YESU alikufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu. Alichukua vazi letu lililochafuliwa na uchafu wa dhambi zetu akatupa vazi Lake takatifu la haki. YESU aliuawa kwa kosa lako na langu. Akatupa haki Yake na kutuambia tusichafue tena maisha yetu.
Kuendelea kutenda dhambi baada ya yale ambayo Yesu ametufanyia ni kuidharau sana kazi ya msalaba na kuikanyagia chini Damu Yake ambayo tumesafishwa kwayo.
Ni kushindwa kuthamini kuwa kuna mtu alishakufa kwa ajili yetu. Ni kushindwa kutambua uthamani wa wokovu ambao tumeupokea.
Wapendwa,
*Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii?*
T A F A K A R I
Updated at: 2024-07-16 11:49:06 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Karibu kwa Ibada ya Jumapili ya Huruma ya Mungu! Leo tunajikita katika kupata upendo usiokuwa na kifani kutoka kwa Mungu wetu mwenye huruma. Kama Wakatoliki, tunajua umuhimu wa ibada hii katika maisha yetu ya kiroho kwa sababu ni siku maalum ambayo kwayo tunapata msamaha na uponyaji kutoka kwa Mungu wetu.
Kwa nini tunahitaji upendo usiokuwa na kifani katika maisha yetu? Kwa sababu upendo huu ni wa kweli, una nguvu, na unaweza kusuluhisha matatizo yote katika maisha yetu. Tunahitaji upendo usiokuwa na kifani ili tuweze kuwa na maisha yenye furaha na amani.
Katika Biblia, tunaona upendo usiokuwa na kifani wa Mungu kwa binadamu katika Yohana 3:16, "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele." Hii inaonyesha kuwa Mungu anatupenda sana hata kutupa Mwana wake pekee ili tuweze kuokolewa.
Kupitia Ibada ya Jumapili ya Huruma ya Mungu, tunaweza kumwomba Mungu atupe upendo wake usiokuwa na kifani, tunaweza pia kuomba msamaha wa dhambi zetu na kuponywa kutoka kwa magonjwa na hata maumivu ya moyo. Kwa sababu Mungu wetu ni mwenye huruma, yeye atatusikia na kutujibu.
Kama Wakatoliki, tunajua umuhimu wa huruma katika maisha yetu. Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, huruma ni "upendo wa kujitoa bila masharti, unaotokana na Mungu." (CCC 1829). Tunapaswa kuwa na huruma kwa wengine kama Mungu anavyotuonyesha huruma yake. Hii inamaanisha kuwa tunapaswa kuwakaribisha wengine, kuwasaidia na kuwatunza, hata wakati wanatukosea.
Tunaweza pia kujifunza kutoka kwa watakatifu wetu, hasa Mtakatifu Maria Faustina Kowalska, ambaye alikuwa na uhusiano mzuri na Mungu wa huruma. Katika Diary yake, Mtakatifu Maria Faustina alisema, "Mungu hawezi kutenda tofauti kwa yule ambaye anapenda kwa kweli, bali kwa hiyo hiyo anamtendea yule ambaye anampenda kwa upendo wake mkamilifu." Kwa hiyo, tunaweza kumwomba Mungu kupitia Ibada ya Jumapili ya Huruma ya Mungu ili atupatie upendo wake usiokuwa na kifani na tutumie upendo huo kuwakaribisha wengine.
Kwa ufupi, Ibada ya Jumapili ya Huruma ya Mungu ni siku muhimu katika maisha yetu ya kiroho. Tunapata upendo usiokuwa na kifani kutoka kwa Mungu wetu mwenye huruma, tunapata msamaha na uponyaji kutoka kwa dhambi zetu na tunajifunza kuwa na huruma kwa wengine. Tumwombe Mungu wetu mwenye huruma kupitia Ibada hii ili atutie moyo na kutupa nguvu ya kumpenda kwa upendo wake mkamilifu. Je, umewahi kushiriki Ibada hii? Je, umehisi upendo wa Mungu katika maisha yako? Tujulishe katika sehemu ya maoni hapa chini.
Updated at: 2024-07-16 11:49:16 (1 year ago by DIN - Melkisedeck Leon Shine)
Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha umuhimu wa kuheshimu uhuru wa dini na kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali? Ndio! Kanisa Katoliki linapenda kuhimiza kila mtu kuheshimu uhuru wa dini na kuheshimu imani ya wengine, na kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali. Kama Wakatoliki, tunapaswa kuwa mfano wa amani na upendo kwa wengine, hata kwa wale ambao hawana imani yetu.
Katika Injili, Yesu Kristo alipenda kutangaza amani na upendo kwa kila mtu. Yeye alisema katika Mathayo 5:9 "Heri wenye amani, kwa kuwa wao watapewa na Mungu jina lao la kuwa wana." Hii inaonyesha jinsi Mungu anavyopenda amani na upendo, na hivyo tunapaswa kuwa wakazi waadilifu wa dunia hii, wakipenda amani na kuheshimu wengine.
Kanisa Katoliki linafundisha kuwa kila mtu ana haki ya uhuru wa dini na kukubaliwa kwa imani yake, bila kujali ni dini gani. Hii inamaanisha kwamba kila mtu anapaswa kuheshimiwa kwa imani yake na kuheshimu imani ya wengine. Wakatoliki tunapaswa kuwa na heshima ya wengine, hata kama kuna tofauti za kidini.
Kanisa Katoliki linapendekeza kwamba sisi sote tunapaswa kuchangia katika kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali. Hii inaweza kufanywa kwa njia ya majadiliano, kutembeleana, na kushirikiana kwa malengo mema. Kwa mfano, tunaweza kuwaalika wenzetu wa dini nyingine kwa misa zetu au hata kushiriki katika shughuli za kijamii na za kimaendeleo.
Kanisa Katoliki linasema pia katika Catechism of the Catholic Church kwamba "uhuru wa dini unahusisha haki ya kila mtu ya kufuata dhamiri yake katika mambo yote yanayohusiana na dini" (CCC 2106). Hii ni sehemu ya haki ya binadamu ambayo inapaswa kulindwa kote ulimwenguni. Kwa hiyo, kama Wakatoliki, tunapaswa kuongoza kuwa mfano wa kulinda haki hii ya binadamu.
Katika Wagalatia 5:13, Paulo anasema "Kwa maana ninyi, ndugu, mliitwa kwa ajili ya uhuru; lakini msitumie uhuru wenu kuwa sababu ya kufanya mambo maovu, bali tumikianeni kwa upendo." Hii inaonyesha kwamba uhuru unapaswa kutumika kwa njia ya upendo na kuheshimu wengine. Tunapaswa kutumia uhuru wetu kwa kusaidiana kwa upendo na kuheshimiana wengine.
Mwisho, tunahitaji kuwa na ufahamu wa kutosha juu ya dini mbalimbali. Kwa kweli, tunapaswa kujua imani yetu kwa undani, lakini pia tunapaswa kuelewa imani za wengine. Hii itatusaidia kuheshimu imani ya wengine na kuwa mfano wa amani na upendo.
Kwa hiyo, tunapaswa kuheshimu uhuru wa dini na kuheshimu imani ya wengine, kukuza uelewa na amani kati ya dini mbalimbali, na kuwa mfano wa upendo na amani kwa wengine. Neno la Mungu linasema, "Bwana wa amani mwenyewe awape amani kwa njia zote. Bwana na awe pamoja ninyi nyote" (2 Wathesalonike 3:16).