Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kisamvu ni aina ya mboga ya majani inayopatikana kwa wingi na kwa urahisi katika mikoa takriban yote nchini Tanzania. Pia aina hii ya mboga hupikwa katika mapishi ya aina mbalimbali kulingana na mahitaji ya mpishi.
Aina hii ya mboga kama zilivyo mboga zingine za majani ni nzuri na muhimu kwa afya ya binadamu. Aina hii ya mboga huleta virutubisho mbalimbali mwilini. Hapa tunaenda kuona mapishi ya kisamvu kwa kutumia mafuta bila nazi kama ilivyozoeleka na wengi.
Mahitaji :
• Kisamvu kilichotwangwa na kuwa laini • Kitunguu maji • Kitunguu swaumu • Kunde mbichi • carrots • Mafuta ya kula • Chumvi kiasi
Maandalizi :
• Chemsha kisamvu ukiwa umechanganya na kunde mpaka uhakikishe vyote vimeiva. Baada ya kuiva weak pembeni. • Chukua sufuria kavu, weak mafuta kasha weak katika jiko na yakipata moto weak kitunguu na koroga mpaka kibadilike rangi kasha weak kitunguu swaumu na endelea kukoroga kwa muda baada ya hapo weak carrots na kisha weka kisamvu chako ambacho kimechanganywana kunde. • Endelea kukoroga kwa muda na kasha acha kichemke mpaka uhakikishe mboga yako imeiva vizuri. • Mboga hii iko tayari kwa kulikwa na inaweza ikaliwa na wali au ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage (beans 2 vikombe vya chai) Nazi (coconut milk kiasi) Vitunguu maji (onion 1kikubwa) Nyanya (fresh tomato 1) Kitunguu swaum (garlic paste 1/4 kijiko cha chai) Chumvi (salt kiasi) Curry powder 1 kijiko cha chai Mafuta (vegetable oil)
Matayarisho
Chemsha maharage mpaka yaive kisha yaweke pembeni. Kaanga vitunguu maji na mafuta mpaka vianze kuwa vya brown kisha weka kitunguu swaum,nyanya na curry powder. kaanga mpaka nyanya iive kisha tia maharage na chumvi kiasi. Geuza mpaka mchanganyiko uchanganyike vizuri. Baada ya hapo tia tui la nazi na ukoroge vizuri na uache lichemke mpaka liive. Baada ya hapo ipua na maharage yatakuwa tayari kwa kuliwa
Jinsi ya kupika Biriani ya Nyama Ng'ombe Na Mtindi
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Mchele wa biriani - 5 gilasi
Nyama ya ngombe ya mifupa - 1 ½ kilo na nusu
Vitunguu - 2 kilo
Tangawizi mbichi - ¼ kikombe
Thomu (saumu/garlic) - 3 vijiko vya supu
Mtindi - 2 vikombe
Nyanya ilokatwakatwa (chopped) - 3
Nyanya kopo - 1 kikombe
Masala ya biriani - 2 vijiko vya supu
Hiliki ya unga - 2 vijiko vya chai
Pilipili mbichi ilosagwa - 3 kiasi
Kotmiri ilokatwakatwa - 1 msongo (bunch)
Rangi ya biriani ya manjano - ½ kijiko cha chai
Zaafarani au zaafarani flavour - 1 kijiko cha supu
Mafuta ya kukaangia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Katakata vitunguu ukaangae katika mafuta mpaka vigeuke rangi ya brown ilokoza. Weka nyama iwe ilokatwakatwa katika treya au bakuli kubwa la oveni. Chaganya pamoja na tangawizi, thomu, nyanya, nyanya kopo, mtindi, masala ya biriani, chumvi, pilipili. Acha irowanike kwa muda wa masaa mawili takriban. Funika kwa karatasi ya jalbosi (foil paper) utie katika oveni upike muda wa dakika 45 takriban mpaka nyama iwive na huku unachanganya changanya sosi. Ikiwa ina maji ongezea nyanya kopo iwe nzito. Epua funua, kisha vuruga vitungu umwagie pamoja na kotmiri na umwagie mafuta ya moto kiasi. Ongezea kutia masala ya biriani na hiliki ya unga. Chemsha mchele nusu kiini, mwaga maji chuja, umwagie juu ya sosi ya nyama ukipenda kuchanganya au chemsha wali pekee. Nyunyizia rangi ya biriani pamoja na zaafarani flavour au zaafarani yenyewe ukipenda. Mimina mchele juu ya masala ya nyama, funika urudishe ndani ya oven upike muda wa kiasi ya dakika ishirini. Epua upake kwa kuchota wali kwanza kisha masala uwekee juu yake, kiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Tambi (vermiceli Roasted) Mifuko 2
Siagi - 4 Vijiko vya supu
Maziwa (condensed) 300Ml
Lozi zilizokatwakatwa - 1 kikombe
Zabibu kavu - 1 Kikombe
Arki (essence) - 1 Kijiko cha supu
MAPISHI
Weka karai kwenye moto kiasi Tia siagi Tia tambi uzikaange usiachie mkoni mpaka ziwe rangu ya dhahabu. Weka lozi na zabibu huku unakoroga Tia maziwa na huku unakoroga usiachie mkono. Tia arki Epua karai, tumia kijiko cha chai kwa kuchotea na utie kwenye kikombe cha kahawa nusu usikijaze. Kipindue kwenye sahani utoe kileja. Fanya hivyo mpaka umalize vyote.
Jinsi ya kutengeneza Cookies Za Tende Na Tangawizi
Updated at: 2024-05-25 10:34:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga vikombe vikombe 4
Baking soda 1 kijiko cha chai mfuto
Siagi 400 gms
Sukari ½ kikombe
Tende chambua ukatekate ifikie ¾ kikombe
Tangawizi ya unga vijiko 2 vya chai
Vanilla 1 kijiko cha chai
Yai 1
Maziwa mazito vijiko 2 vya kulia.
MAANDALIZI
Changanya siagi na sukari katika mashine usage mpaka iwe laini nyororo. Tia yai uchanganye vizuri Tia tende na vanilla, tangawizi uchanganye vizuri. changanya unga na baking soda kisha, mimina kidogo kidogo huku unachanganya kwa kijiko cha ubao (mwiko). Unga ukiwa mzito ongeza vijiko 2 vya maziwa. Fanya viduara upange katika treya uliyopakaza siagi kisha uchome (bake) katika over moto mdogo wa kiasi dakika 15 vigeuke rangi viwive. Epua vikiwa tayari
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi tamu (plantain) 3-4 Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai
Matayarisho
Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Matunda ni mojawapo wa kundi la vyakula, ni muhimu sana kwa afya bora. Matunda yakitengenezwa vizuri yanavutia sana na yanakuwa ni chakula kizuri sana.
Mahitaji
Embe iliyoiva kiasi Nanasi Tango Tikiti maji Zabibu Papai
Matayarisho
1. Ondoa maganda kwenye embe, nanasi, tango, papai na tikiti maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba
2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake.
3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo
4. Saladi yako tayari kwa kuliwa
Waweza kula saladi hii kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Unga wa ngano (self risen flour 2 vikombe vya chai) Hamira (yeast kijiko 1 cha chai) Sukari (sugar 2 vikombe vya chai) Hiliki (cardamon 1/4 ya kijiko cha chai) Maji kikombe1 na 1/2 Mafuta
Matayarisho
Changanya unga, hamira, maji na mafuta kijiko 1. Koroga vizuri mpaka upate uji mzito usiokuwa na madoge Baada ya hapo uache uumuke kisha zichome kalmati katika moto wa wastani. Baada ya hapo tia sukari, hiliki na maji 1/2 kikombe katika sufuria na ichemshe uku unakoroga mpaka iwe tayari.(ukitaka kujua kama iko tayari chovya mwiko kisha gusa na vidole utaona iko kama nta au gundi) Baada ya hapo tia kalmati na uzichange pamoja mpaka zikolee kisha zitoe na uziache mpaka zipoe tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ng’ombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.