Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:43 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Viazi (potato) 1 kilo Nyama ya ng'ombe 1/2 kilo Nyanya ya kopo iliyosagwa 1/2 tin Vitunguu maji 2 Tangawizi/ swaum 1 kijiko cha chai Hoho 1 Curry powder 1 kijiko cha chai Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Limao 1/2 Chumvi Coriander Mafuta ya kupikia
Matayarisho
Safisha na katakata nyama ktk vipande vidogovidogo kisha weka pembeni. Baada ya hapo kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown kisha tia nyama, swaum/ tangawizi, chumvi na limao. Ichanganye vizuri kisha funika na uipike mpaka iive na maji yote yakauke yani yabaki mafuta tu. Baada ya hapo tia viazi vilivyokatwa vipande vya wastani vikaange kwa muda wa dakika 10 kisha tia pilipili na curry powder na nyanya. Funika na punguza moto.Pika mpaka nyanya iive vigeuze kisha tia vimaji kidogo vya kuivishia viazi. Viazi vikikaribia kuiva(hakikisha vinabaki na rojo kidogo) tia hoho na upike kwa muda wa dk 5 kisha malizia kwa kutia coriander. Changanya vizuri kisha ipua na viazi vyako vitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI VYA TUNA
Tuna (samaki/jodari) - 2 Vikopo
Vitunguu (kata kata) - 4
Nyanya zilizosagwa - 5
Nyanya kopo - 3 Vijiko vya supu
Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo - cubes) - 4
Dengu (chick peas) - 1 kikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Hiliki - 1/4 kijiko cha chai
Mchanganyiko wa bizari - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - 1 Kijiko cha chai
Vipande cha Maggi (Cube) - 2
VIAMBAUPISHI VYA WALI
Mchele - 3 Vikombe vikubwa (Mugs)
Mdalasini - 2 Vijiti
Karafuu - chembe 5
Zaafarani - kiasi Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) - 1/2 Kikombe
JINSI YA KUANDAA
Kosha Mchele na roweka. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando. Kaanga viazi, epua Punguza mafuta, kaanga nyanya. Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi. Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi. Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu. Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika chombo cha kupikia katika jiko (oven) Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali. Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu). Funika wali na upike katika jiko moto wa 450º kwa muda wa kupikika wali. Epua upakue.
Updated at: 2024-05-25 10:34:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
MAHITAJI
Unga - 2 Vikombe Sukari ya icing - 1 Kikombe Siagi - 250 gm Yai - 1 Vanilla - 2 Vijiko vya chai Baking powder -1 Kijiko cha chai Jam - ¼ kikombe Lozi - ¼ kikombe
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia yai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini kama sufi. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Chota mchanganyiko kwa mkono (kiasi cha kijiko kimoja cha supufanya duara kisha weka kwenye treya ya kupikia. Bonyeza kila kiduara katikati kwa kidole, kisha weka jam na tupia lozi zilizomenywa na kukatwa katwa. Pika (bake) katika oven moto wa 375° F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi tamu (plantain) 3-4 Tui la nazi (coconut milk) kikombe 1 cha chai Sukari (sugar) 1/4 ya kikombe cha chai Hiliki (Ground cardamon) 1/4 ya kijiko cha chai Chumvi (salt) 1/4 ya kijiko cha chai
Matayarisho
Menya ndizi kisha zikwangue utomvu wote. Baada ya hapo zikate kati (kiurefu) na kisha kata tena kati katika kila ndizi vitoke vipande 4. baada ya hapo toa moyo wa katikai wa ndizi. Zioshe na kisha zikaushe maji na uziweke kwenye sufuria ya kupikia. Baada ya hapo tia tui la nazi, sukari, chumvi na hiliki. Ziinjike jikono na uziache zichemke uku ukiwa unalikoroga tui ili lisikatike. Baada ya dakika 10 tui la nazi litakuwa limepungua na kubaki kidogo na hapo ndizi zitakuwa zimeshaiva. Ziache zipoe na zitakuwa tayari kwa kuliwa. Zinaweza kuliwa kama mlo (main meal) au kitinda mlo (dissert) au mlo wa pembeni (side dish) haswa kwa futari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:52 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Viamba upishi
Maziwa ya unga 2 vikombe
Sukari 3 vikombe
Maji 3 vikombe
Unga wa ngano ½ kikombe
Mafuta ½ kikombe
Iliki kiasi
Jinsi ya kuandaa na kupika
Paka sinia mafuta kabla ya kupika labania Katika sufuria chemsha maji na sukari pamoja na iliki mpaka inate vizuri Kisha mimina mafuta koroga Halafu mimina unga wa ngano na ukoroge haraka haraka Kisha tia unga wa maziwa, endelea kukoroga usiwe na madonge mpaka uwe rangi ya browni isiokoleza. Kisha mimina mchanganyiko kweye sinia uliyoipaka mafuta, iwache ipoe na kata kata upendavo na itakuwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:34:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Vipimo
Ndizi mbichi - 10
Nyama - kilo 1
Nazi ya kopo - 1
Chumvi - 1 Kijiko cha chakula
Ndimu - 1
Bizari ya manjano - 1 Kijiko cha chai
Pili pili mbichi - 3
Nyanya (tomatoes) - 2
Kitunguu maji - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chakula
Namna ya Kutayarisha Na Kupika
Kata nyama vipande vipande na uisafishe. Chemsha nyama weka chumvi, thomu, tangawizi na ndimu. Iache iwive. Kata kata nyanya na kitunguu, kisha mimina kwenye nyama inayochemka, weka na bizari nusu kijiko. Wacha supu iwive kisha weka pembeni. Ukumbusho: Hakikisha supu inakuwa kiasi na si nyingi. Menya maganda ndizi na uzikate vipande vipande vya kiasi. Zikoshe ndizi na uziweke ndani ya sufuria. Weka maji ndani ya sufuria kisha zichemshe ndizi mpaka ziwe laini kidogo. Zimwage maji ndizi kisha mimina supu na nyama ndani ya ndizi. Mimina nazi pili pili na bizari nusu kijiko ndani ya ndizi na uziweke kwenye jiko zichemke mpaka zibakie na urojo kiasi. Onja chumvi na uongeze kadri utakavyopenda. Weka pembeni zipoe. Pakua ndizi kwenye sahani au bakuli tayari kwa kuliwa.
Loweka mchele kwa muda wa dakika 10 na uchuje maji yote kisha chemsha maji ya moto na uweke pembeni. Kisha tia mafuta kiasi katika sufuria na ukaange vitunguu, carrot na njegere pamoja. kwa muda wa dakika 5 baada ya hapo tia turmaric na chumvi. pika kwa muda wa dakika 5 na utie mchele na maji ya moto kiasi funika na upike mpaka uive. Chemsha kuku pamoja na limao, chumvi, kitunguu swaum na tangawizi mpaka aive kisha mweke pembeni. Saga pamoja kitunguu,kitunguu swaum, tangawizi na nyanya. Kisha bandika jikoni na uache uchemke bila mafuta mpaka maji ya kauke.Baada ya hapo tia chumvi, mafuta ,curry powder, bilinganya na kuku. Kaanga pamoja kwa muda kisha tia maji au supu ya kuku kwa kukadiria mchuzi uutakao. Acha uchemke mpaka mabilinganya yaive na hapo mchuzi utakuwa tayari kuseviwa na wali.
Updated at: 2024-05-25 10:37:41 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Maharage yaliyochemshwa kiasi Spinach zilizokatwa kiasi Vitunguu maji 2 Nyanya 1/2 kopo Swaum/Tangawizi 1 kijiko cha chakula Curry powder 1 kijiko cha chai Olive oil Chumvi
Matayarisho
Kaanga vitunguu vikianza kuwa vya brown tia tangawizi/swaum kisha nyanya. Pika mpaka nyanya ziive kisha tia curry powder na chumvi. Vipike kiasi kisha tia maharage na maji kidogo kisha funika na uache vichemke. Baada ya muda tia spinach vipike pamoja na maharage mpaka ziive kisha ziipue. Baada ya hapo mboga yako itakuwa tayari kwa kuseviwa.