Madhara ya kumlaza mtoto kifudifudi, kumlaza kwa tumbo
Welcome Back.
Updated at: 2024-05-25 10:35:13 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Unafahamu nini kuhusu suala la kumlaza mwanao? Maana Mapokeo tuliyo yapokea enzi na enzi ni kuwa ukitaka mtoto wako alale bila kushtuka basi alalie tumbo. Bado watu wengi wanaendelea kufanya hivyo hata sasa hivi unaposoma makala haya.
Sayansi inashauri kuwa ni hatari kumlaza mtoto kwa tumbo. Visa kadhaa vya watoto kupoteza maisha vimehusishwa na watoto kulalia tumbo.
Kuanzia mwaka 1992 Madaktari wa watoto nchini Marekani walipendekeza kuwa watoto wachanga walale chali ( walalie Mgongo) ili kuepuka vifo vya ghafla vya watoto. Kifo cha ghafla hutokea pale ambapo mtoto mchanga anakutwa amefariki akiwa usingizini.
Tangu pendekezo hilo la madaktari idadi ya vifo vya ghafla vya watoto imepungua zaidi ya nusu ya vifo vyote vya watoto vinavyotokea wakiwa usingizini.
Ni vizuri kuhakikisha kuwa kila mtu anayekusaidia kulea mtoto anajua jinsi ya kumlaza mtoto chali.
Hata hivyo kuna baadhi ya watoto unaweza kushauriwa na daktari iwapo mwanao usimlaze chali na alalie tumbo.
Updated at: 2024-05-25 10:35:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mwanamke anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.
"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi”
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite.”
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.
"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,”
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebish a na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
Updated at: 2024-05-25 10:35:21 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Leo nimekuletea matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la parachichi.
Kwanza mbegu ya parachichi huweza kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho 'antioxidants' hii ni kutokana mbegu hiyo na kuwa na zaidi ya asilimia 70 ya kirutubisho hicho.
Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanyika mwaka 2004 chini ya chuo kikuu cha Singapore na kuchapishwa katika Food chemistry walibaini kuwa mbegu hiyo inakiwango kikubwa cha antioxidants ikiwa ni pamoja na mbegu za matunda mengine kama vile embe, stafeli n.k
Mbegu hii ya parachichi pia huweza kuwasaidia wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito kwani matumizi ya mbegu hiyo husaidia kuunguza mafuta mwilini na hivyo kupunguza uzito mkubwa mwilini.
Matumizi ya unga wa mbegu hizo pia husaidia kupunguza shida ya maumivu ya mwili hasa kwenye maungio yaani 'joint' za mwili.
Lakini pia kwa wenye shida ya maumivu ya viungo hivyo wanashauriwa kutumia hata mafuta ya parachichi yenyewe kwani huweza kutoa ahueni kwa haraka zaidi.
Pamoja na hayo pia mbegu za parachichi husaidia kurekebisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula tumboni.
Saga mbegu ya parachichi kisha changanya na maji ya uvuguvugu kisha koroga vizuri na utumie mchanganyiko huo kutwa mara 2 kwa siku kwa muda wa wiki 2 mfululizo.
Updated at: 2024-05-25 10:35:02 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti.
Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.
Watu wengi hufikiri kuwa kula mboga za majani ni umaskini; lakini ukweli ni kuwa mboga za majani zina manufaa makubwa kwenye miili yetu. Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri.
Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).
Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.
Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.
Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.
Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.
Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.
Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.
Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.
Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.
Updated at: 2024-05-25 10:35:23 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu kuwa kufunga kula kuna manufaa ya kiafya pia. Kufunga kula ni tendo lenye historia ndefu sana ambayo kimsingi chimbuko lake ni sababu za kiimani. Hata hivyo shuhuda na tafiti mbalimbali zimedhihirisha kuwa kuna manufaa mengine kemkem ya kufunga kula mbali na yale ya kiimani.
Ikiwa basi unapenda kuongeza maarifa pamoja na kuboresha afya yako, fahamu faida za kufunga kula.
Metaboli ni mchakato ambao mwili hutumia virutubisho kutoka kwenye vyakula ili kujipa nguvu.
Unapofunga kwanza unapumzisha mfumo wako wa umeng’enyaji, pili unaufanya mchakato wa metaboli kwenda vizuri kwani mwili utatumia vyema virutubisho vilivyoko mwilini tayari.
Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kufunga kula hufanya mzunguko wa damu uende vizuri hasa kwa watu wenye aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari (Type 2 Diabetes)
Kufunga kula ni njia mojawapo bora ya kupunguza uzito kwani kwa njia hii mwili hutumia mafuta yaliyoko mwilini ili kujipa nguvu.
Unapofunga kula mwili huzalisha insulini ili kutawala kiwango cha sukari mwilini kwani hakuna sukari inayoingia. Kwa njia hii insulini itaweza kuzalishwa na kufanya kazi ipasavyo mwilini mwako.
Watu wengi wanapofunga hujikuta pia shinikizo la damu likipungua, hii inasababishwa na kupungua kwa kiwango cha chumvi kwenye damu.
Kumbuka chumvi nyingi husababisha shinikizo la damu. Hivyo kufunga ni kupunguza kiasi cha chumvi kinachoingia mwilini.
Kwa watu wenye kiwango kikubwa cha sukari mwilini, wanaweza kutumia njia ya kufunga ili kukipunguza. Kumbuka unapofunga unapunguza pia kiwango cha sukari kinachoingia mwilini.
Watafiti wa afya wanaeleza kuwa kula sana kunakufanya pia uzeeke mapema. Wanaeleza kuwa kula kidogo kutatawala mchakato wa metaboli, hivyo kuzuia seli kuchakaa mapema.
Kuna watu huwa wanashindwa kula vizuri kwa sababu huwa hawahisi njaa vyema. Njia moja wapo ya kupata njaa ambayo itakusababisha ule vyema, ni kufunga kula.
Kufunga kula kunachochea uzalishaji wa protini ya brain-derived neurotrophic factor (BDNF) ambayo ni muhimu sana katika ukuaji, afya na utendaji kazi wa seli za fahamu za ubongo (neurons).
Kufunga kula hufanya kinga mwili kujiimarisha ili kukabiliana na chochote kinachoweza kutokea.
Hii ni kwa sababu unapofunga unabadili hali ya msingi ya mwili na inabidi kinga mwili kujiimarisha kujianda na lolote linalohusiana na mabadiliko hayo.
Ingawa lishe bora ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi, kufunga kula kunaifanya ngozi iwe na mwonekano mzuri.
Ngozi inapokuwa na sukari nyingi, huifanya iwe na mwonekano usiovutia.
Kwa kufunga kula utapunguza kiwango cha sukari kinachoingia mwilini, hivyo kuwa na ngozi yenye mwonekano mzuri.
12. Huwezesha kujizalisha upya kwa seli
Seli hukua na kuchakaa au hata kufa kwenye mwili wa binadamu. Kama ilivyo kwa kinga mwili, utafiti unaonyesha kuwa unapofunga mwili huzalisha seli mpya ili kujiaanda au kukabili badiliko lolote linaloweza kutokea.
Watafiti wa afya wanaeleza kuwa kufunga kula kunasababisha mishipa ya moyo na misuli kufanya kazi vyema.
Njia nzuri ya kutawala umbo au mwonekano wako ni kwa kutawala kile unachokula. Hii ndiyo sababu walimbwende au warembo hujizuia sana kula hovyo ili wasije wakaharibu mwonekano wao.
Kwa njia ya kufunga kula utaweza kutawala umbo na mwonekano wa mwili wako kama unataka uwe mnene au mwembamba.
Hakikisha unafunga kwa kuzingatia kanuni za afya pamoja na hali ya afya ya mwili wako. Kama hujawahi kufunga, unaweza kuanza taratibu au kwa kupunguza kiasi cha mlo wako hadi utakapozoea.
Ikiwa unatatizo la kipekee la afya, ni vyema ukapata ushauri wa daktari kwanza.
Updated at: 2024-05-25 10:35:04 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’, ‘Magnesium’ na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction).
Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
Tikitimaji lina kirutubisho aina ya ‘arginine’, ambacho huchochea uzalishaji wa ‘nitric oxide’ kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa ya Viagra.
Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya ‘Potassium’ kama vile Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.
Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji.
Kirutubisho cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili.
Kuondoa ‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
Tunda hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.
Updated at: 2024-05-25 10:35:10 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengi wanapotaka kuota meno humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.
Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.
·Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ute utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.
·Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka.
·Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.
·Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote
·Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza vizuri
Updated at: 2024-05-25 10:37:53 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla. Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni uondoa haiba ya kupendwa kwani hata unapoongea wengi watakwepa kuongea moja kwa moja na wewe kwa sababu ya harufu mbaya inayotoka mdomoni mwako.
Chakula unachokula kina athiri hewa inayotoka mdomoni au sehemu nyingine za mwili wako. Baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu unayotoa mdomoni. Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba atakuambukiza.
Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90% ya tatizo la harufu mbaya mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).
Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya protein. Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).
Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya mdomoni. (Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya chakula). Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa upumuaji na kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na madawa (medications) Kuvuta sigara, kunywa kahawa, ulaji wa vyakula vyenye viungo vikali kama vile vitunguu maji au thaumu.
Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).
Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine. Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu unayemuamini.
Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa, wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.
Kula vyakula vyenye afya na vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza kusafisha kinywa vizuri. Kusafisha meno mara kwa mara au kwa uchache mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, hii usaidia kuondoa au kujikinga na harufu mbaya mdomoni. Vilevile unashauriwa kutumia KISAFISHA ULIMI (tongue cleaner) kusafishia ulimi wako. Tumia bazooka (chewing gum) ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye kimywa kilichokauka. Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha harufu mbaya. Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya kulala usiku. Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa au kila baada ya miezi sita kwa uchache.
Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.
Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.
Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo linalotibika.
Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa makini muongozo ufuatao:
Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua vizuri.
Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila ulalapo. Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.
Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).
Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.
Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.
Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka (chewing gum) yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria.
Hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.
Updated at: 2024-05-25 10:35:03 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Hypotension ndio jina linalotumika kuelezea presha ya kushuka ambayo mpaka sasa chanzo chake hakijawa wazi. Kipimo cha presha huwa na namba mbili. Namba moja huwa juu na nyengine huwa chini. Hivyo basi namba ya juu kikawaida kwa mtu mzima inapaswa kuwa 100 hadi 139 na ya chini inapaswa kuwa 60 hadi 90. Hivyo basi pressure yako ikiwa chini ya 100/60 Ndio inajulikana kama Hyptension yaani pressure iko chini. Hypotension (haipo juu). Kwa watu wengi presha hii huwatia kizunguzungu na kuwaangusha. Presha hii ikiwa ya muda mrefu husababisha mtu kupata maradhi ya mshtuko.Watu wenye afya nzuri, hasa wakimbiaji, presha ya kushuka huwa ni dalili ya uzima kwao. Si rahisi kuziona dalili kwa mtu mwenye presha ya kushuka hata kama imedumu kwa muda mrefu. Mara nyingi matatizo ya kiafya huonekana pale mtu presha yake inaposhuka ghafla. Wakati huo wa matatizo ya kiafya, damu kidogo hufika katika ubongo. Hali hii humfanya mtu awe na kizunguzungu au kuumwa na kichwa. Kushuka ghafla kwa presha mara nyingi humtokezea mtu pale anapofanya jambo la haraka kama mtu aliyekaa na kutaka kusimama mara moja. Kitaalamu presha hii inajulikana kama postural hypotension, orthostatic hypotension, au neurally mediated orthostatic hypotension. Postural hypotension inachukuliwa ni hali ile ya kushindwa kwa mfumo wa mawasilianao unaojiendesha wenyewe mwilini kufanya kazi yake kikamilifu (autonomic nervous system). Mfumo huu huendesha na kuongoza vitendo visivyo vya hiari (involuntary vital actions), kama vile mapigo ya moyo kubadilika kutokana na jambo lililotokea kwa wakati uleopo. Kwa kawaida unapoinuka, kiwango fulani cha damu yako kinakuwa kimebaki sehemu ya chini (miguuni). Kukiwa hakuna hatua yeyote iliyochukuliwa na mwili wako, hali hii itasababisha presha yako kushuka. Katika hali hii mwili wako unafanya nini ? Mwili wako unapeleka taarifa kwenye moyo na kuamuru uongeze usukumaji wa damu ambao utaizidi mishipa yako na kuifanya kuwa membamba hali itakayopelekea kuifanya presha yako kubakia ileile. Ikiwa jambo hili halikufanyika au limaefanyika polepole sana, presha yako itashuka ghafla. Hapa ndipo mtu unapomuona anaguka ghafla. Kwa ufupi athari ya maradhi ya presha ya kushuka na ya juu huongezeka kadri mtu anapokuwa na umri mkubwa na pia kubadilikabadilika kadri umri unavyoongezeka. Jambo jingine la kufahamu ni kuwa, ufikaji wa damu kikawaida kwenye ubungo unapungua kadri umri unavyoongezeka. Inakisiwa kiasi cha asilimia 10 mpaka 20 ya watu wenye umri unaozidi miaka 65, wanapata tatizo la presha yao kushuka.
Updated at: 2024-05-25 10:35:00 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Uti wa mgongo ulio wazi( Spinal bifida) ni hali ambayo mtoto anazaliwa nayo huku uti wa mgongo (mishipa ya fahamu mkubwa unaotoka kwenye ubongo) ukiwa wazi kutokana na mifupa (vipingili vya uti wa mgongo) kutokufunga vizuri.
Mgongo wazi(spinal bifida) inaweza pata watoto 3 kati ya watoto 10000 wanaozaliwa.
Uti wa mgongo hutengenezwa mara tu baada ya mimba kutungwa, ikiwa kuna kasoro katika utengenezaji wa uti huu basi sehemu fulani ya uti wa mgongo itabaki bila kuzibwa.
Kuna sababu mbalimbali zinapelekea uti wa mgongo kutoziba, ambazo zinaweza zuhilika, nazo ni Upungufu wa folic acid(vit B9) na vitamin B12 katika kipindi cha ujauzito, katika kipindi cha miezi ya awali.
Mama mjamzito kupiga X-ray, mattumizi ya dawa za kifafa katika kipindi cha ujauzito .
Pamoja na maambukizi ya baadhi ya virusi kwa mama mjamzito.
Zipo aina mbiliza tatizo la tundu katika mgongo ama mgongo wazi
Aina ya kwanza ni occulta ambapo huwa na aina mbili pia, aina ya kwanza ni ile ambapo panakuwa na vinyweleo tu vinavyoonekana nyuma chini ya mgongo bila kuwa na dalili zozote zile, ama kunaweza kujitokeza kwa kuta zinazofunika mishipa ya fahamu tu.
Aina ya pili ni ni cystica ambapo panakuwa na vifuko vinavyofunika mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya kuchomoza katika tundu la mgongoni.
Aina hii ni mbaya zaidi kwani linaweza kusababisha mtoto asitembee ama asiweze kuzuia haja kubwa na ndogo.
Dalili huwa kama zifuatazo
Kuwa na uvimbe nyuma chini ya mgongo.
Kuwa na vinyweleo sehemu za chini za mgongo bila kuwa na tatizo la mishipa ya fahamu
Kushindwa kutembea ama kukosa hisia katika miguu
Mtoto anaweza kushindwa kuzuia haja kubwa ama ndogo endapo mishipa yote ya fahamu imepita katika tundu hilo.
Na dalili zingine zinazoambatana kuharibika kwa mishipa.
Upasuaji
Upasuaji ni tiba pekee ya uti wa mgongo ulio wazi(spinal bifida) inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa mishipa ya fahamu(neurosurgeons) wanachofanya ni kuziba lile tundu lililowazi.
Wanawake wengi walio katika kipindi cha kuzaa na wajawazito hawatumii vyakula vyenye vitamin B na folic acid inavyopaswa, vyakula hivyo ni matunda,mboga za majani, mbaazi na choroko.
Mwanamke mjamzito akipata lishe yenye virutubisho hivyo pamoja na kunywa vidonge vya folic acid, kwa asilimia 30% inaweza kupunguza hatarishi ya kupata watoto wenye uti wa mgongo ulio wazi.
Pia kwa wanawake wajawazito katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo, wanashauriwa kutokupiga X-ray.Inawezekana mwanamke akawa hatambui kama ni mjamzito,kipimo cha mkojo cha ujauzito(UPT-urinary pregnancy test) kifanyike kwa haraka kama mwanamke haelewi vizuri mzunguko wake wa hedhi kabla hajapiga X-ray ikiwa ana tatizo lingine la kiafya,
Mwanamke mwenye kifafa akiwa mjamzoto pia yupo kwenye matibabu, awahi haraka kwa daktari kushauriana ni nini zaidi cha kufanya ili kumsaidia.
Wanawake wajawazito wanashauriwa kuhudhulia kliniki mapema zaidi ili wapate elimu ya lishe na kuweza kuanza mapema kutumia folic acid kama kinga ya Mgongo wazi.
Jamii inapaswa kujua kuwa Mgongo wazi(Spinal bifida) haitokani na mambo ya kishirikina bali ni hali ambayo inaweza kuzuilika. Mzazi yeyote mwenye mtoto mwenye Mgongo wazi anashauriwa ampeleke mtoto wake hospitali ili apate maelekezo ni wapi mtoto anaweza kupata matibabu ya upasuaji.)