BADILIKA : huu ni mwaka mpya
"Umasikini hauji kwa bahati mbaya kama ubaguzi wa rangi au ukoloni, umaskini hutokana na matendo ya kila siku ya mwanadamu" (Nelson Mandela, R.I.P)
"Kila mtu anataka kufanikiwa, lakini si kila mtu yuko tayari kushika majukumu na wajibu wa kumpeleka kwenye mafanikio"(Mwl Nyerere, R.I.P).
20 - 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.
25 - 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.
30 - 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.
Ili kutoka hapo ULIPO uweze kwenda HATUA inayofuata kuna SWALI muhimu sana unahitaji kujiuliza.
Watu ambao huwa wanashindwa kupiga hatua katika maisha yao ni kwa sababu huwa wanajiuliza kinyume cha swali hili.
Swali hili ndilo wanalojiuliza watu wote waliofanikiwa:
Swali: "Hivi kwa sasa nina nini ambacho naweza kuanza kukitumia kama mtaji wa kwanza kuanza kufanya ninachotaka"?
Ikiwa leo ni tarehe **1/12 huwezi amini kuwa hakuna tarehe 1 nyingine tutakayoiona ya mwaka huu hivyo sichelei kusema kuwa mwaka umeisha .Lakini mwaka unaishaje??? pengine hili ndilo swali gumu na la muhimu la kujiuliza .Je, Mwaka unaisha ukiwa umefanya nini cha kujipongeza??? .Je mwaka unakaribia kuisha maarifa yako yakiwa yameongozeka kwa kiasi gani???.Haya ni maswali muhimu sana unavyooanza kufikiria juu ya sherehe za mwisho wa mwaka.
Tupo kwenye dunia ambayo tulikuta watu na tutawaacha watu.
Vyote tulivyovikuta vilianzishwa na binadamu wengine wenye mawazo mema na wenye mawazo mabaya pia. Vitu vingi tunavyovifanya tunaendeleza tulivyovikuta ni mara chache kukuta kitu kipya ambacho hakitegemei mazingira na asili ya tulivyovikuta.
1. Usikope pesa ya riba ili uanzishe biashara.
Usitegemee pesa ya mkopo kuianzishia biashara, upate faida kisha uirudishe pesa ya mkopo na riba yake.
2. Usitumie pesa ambayo bado haipo mikononi mwako.
Wala usije ukamuahidi mtu kumpa pesa ambayo umeahidiwa mahali fulani.
Kwenye maisha fursa moja tu inatosha kabisa
kubadilisha hali yako ya sasa na kukuweka kwenye
kiwango kingine kabisa cha mafanikio.Kuna watu
wengi sana ambao waliwahi kufikiria kuwa maisha
yao yatachukua miaka mingi sana kabla
hayajabadilika na kwa mshangao wao walipoanza
kufanya vitu sahihi wakakutana na mabadiliko
makubwa sana katika maisha yao kwa kupitia
fursa moja tu.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba ukiajiriwa maana yake umeshindwa kujitegemea kwa ujuzi wako (yaani hujui ufanyie nini) hivyo umeona uukabidhi ujuzi wako kwa wenye "akili na uwezo" wa kuupangia matumizi ya huo ujuzi wako.
Ndio maana licha ya kwamba elimu ni yako wewe, maarifa ni yako wewe, vyeti ni vyako wewe; na kazi unafanya wewe; lakini hao waliokuajiri ndio wanakuamulia kiasi gani wakulipe! Si hivyo tu bali pia wanao uhuru wa kukupiga mkwara, kukutishia na hata kukufukuza muda wowote (utakapowakosea, watakapojisikia ama watakapokuchoka)! Nini nakwambia? Kama umeajiriwa, usiridhike wala usibweteke na mshahara pekee kwa 100%, hebu jiongeze aiseee, una uwezo wa kuzalisha zaidi sambamba na mshahara (waliojisikia) kukulipa.