Log in to access your menu with tools for managing 📝 tasks, 👥 clients, 💰 finances, 📖 learning, 🔍 personal growth, and 🌟 spirituality, all in one place!.
Welcome to AckySHINE, your go-to platform for personal growth, productivity, and well-being, offering tools tailored to organize your life, manage finances, and deepen your journey.
Updated at: 2024-05-25 10:37:42 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Bamia (okra) 20 Nyanya chungu (garden eggs) 5 Magadi soda (Bicabonate soda) 1/4 ya kijiko cha chai Nyanya (fresh tomato) 1 Chumvi (salt) kidogo Pilipili 1/4
Matayarisho
Osha bamia, nyanya chungu na nyanya kisha vikatekate katika vipande vidogovidogo. Baada ya hapo vitie kwenye sufuria na vitu vyote vilivyobakia na kisha tia maji kidogo.Chemsha mpaka bamia na nyanya chungu ziive na vimaji vibakie kidogo sana. Baada ya hapo ziponde na mwiko kidogo kisha zikoroge na uipue na mlenda utakuwa tayari kwa kuliwa na ugali.
Updated at: 2024-05-25 10:23:07 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI
Unga 3 Vikombe
Sukari ya unga (icing sugar) 1 Kikombe
Siagi 250 gm
Mayai 3
Vanilla 2 Vijiko vya chai
Baking powder 1 Kijiko cha chai
JINSI YA KUPIKA
Koroga siagi na sukari katika mashine ya keki (cake mixer) mpaka iwe laini (creamy). Tia mayai na vanilla koroga mpaka mchanganyiko uwe laini. Tia unga na baking powder changanya na mwiko. Tengeneza round upange kwenye tray utie nukta ya rangi. Nyunyuzia sukari juu ya hizo round ulizotengeneza kabla huja choma. Pika (bake) katika oven moto wa 350°F kama muda wa dakika 15 hivi huku unazitazama tazama.
Updated at: 2024-05-25 10:23:11 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
VIAMBAUPISHI VYA TUNA
Tuna (samaki/jodari) - 2 Vikopo
Vitunguu (kata kata) - 4
Nyanya zilizosagwa - 5
Nyanya kopo - 3 Vijiko vya supu
Viazi (vilivyokatwa vipande vidogo - cubes) - 4
Dengu (chick peas) - 1 kikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic)&Tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Hiliki - 1/4 kijiko cha chai
Mchanganyiko wa bizari - 1 kijiko cha supu
Chumvi - kiasi
Pilipili manga - 1 Kijiko cha chai
Vipande cha Maggi (Cube) - 2
VIAMBAUPISHI VYA WALI
Mchele - 3 Vikombe vikubwa (Mugs)
Mdalasini - 2 Vijiti
Karafuu - chembe 5
Zaafarani - kiasi Jirsh (Komamanga kavu au zabibu kavu -raisins) - 1/2 Kikombe
JINSI YA KUANDAA
Kosha Mchele na roweka. Kaanga vitunguu hadi viwe rangi ya hudhurungi (brown) chuja mafuta uweke kando. Kaanga viazi, epua Punguza mafuta, kaanga nyanya. Tia thomu/tangawizi, bizari zote, vipande vya Maggi, nyanya kopo, chumvi. Mwaga maji ya tuna iwe kavu, changanyisha kwenye sosi. Tia zaafarani kidogo katika sosi na bakisha ya wali. Chemsha mchele pamoja na mdalasini na karafuu. Karibu na kuwiva, chuja maji utie katika chombo cha kupikia katika jiko (oven) Nyunyizia zaafarani, mwagia vitunguu, viazi, na dengu juu ya wali. Mwagia sosi ya tuna na pambia jirshi (au zabibu). Funika wali na upike katika jiko moto wa 450º kwa muda wa kupikika wali. Epua upakue.
Updated at: 2024-05-25 10:34:46 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji:
Unga sembe glass 1 Unga ngano glass 1 Sukari glass 1 (unaweza kupunguza kidogo) Maziwa glass 1 Mafuta 1/2 glass Mayai 4 Iliki iliosagwa 2tbs Bp 2tbs
Jinsi ya kupika:
Saga sukari yako uweke kwenye bakuli safi pamoja na mayai. Tumia mashine ya cake kusagia hadi ifure/ivimbe. Weka mafuta saga, weka maziwa saga, weka unga wa ngano na bp(bp imix kwenye unga kabla kumimina kwenye mchanganyiko) changanya vizuri halafu malizia kwa kuweka unga sembe na iliki usage vizuri.
Chukua trey au sufuria safi weka baking paper Mimina mchanganyiko wako na uoke.
Ukiwiva utoe na uwache upoe. Mkate wa sembe utakua tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:47 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi 6 Nyama ya ng'ombe (nusu kilo) Viazi mviringo 2 Kitunguu swaum Tangawizi Kitunguu maji Nyanya 1 kubwa Mafuta (vegetable oil) Chumvi Limao Pilipili
Matayarisho
Chemsha nyama na limao, kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa
Updated at: 2024-05-25 10:23:15 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - 10-12
Nyama ng’ombe - 1 kilo moja
Kitunguu maji - 2
Nyanya/tungule - 2
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 7
Tangawizi mbichi - 1 kipande
Ndimu - 2 kamua
Chumvi - kiasi
Mafuta - 3 vijiko vya supu
Tui la nazi - 3 vikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Saga kitunguu thomu na tangawiz mbichi. Weka nyama katika sufuria tia kijiko kimoja cha kitunguu thomu na tangawizi, chumvi na ndimu kisha chemsha hadi iive. Menya ndizi ukatekate Weka mafuta katika sufuria tia kitunguu maji kilokatwakatwa ukaange kidogo tu kisha tia nyanya/tungule uendelea kukaanga. Tia tangawizi na thomu ilobakia. Tia ndizi, kaanga kidogo kisha tia supu ya nyama na nyama yake. Ziache ndizi ziive zikiwa tayari tia tui la nazi zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:40 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Tambi (spaghetti 1/2 ya packet) Mafuta (vegetable oil) Sukari (sugar 1/2 kikombe cha chai) Hiliki (cardamon 1/2 kijiko cha chai) Chumvi (salt 1/2 kijiko cha chai) Tui la nazi (coconut oil 1 kikombe cha chai) Maji kiasi
Matayarisho
Tia mafuta kiasi kwenye sufuria kisha ibandike jikoni (katika moto wa wastani) yakisha pata moto kiasi tia tambi na uanze kuzikaanga kwa kuzigeuzageuza kila mara mpaka zitakapokuwa za yangi ya light brown. baada ya hapo ipua na umwage mafuta ya kwenye tambi (bakiza kidogo sana kwani usipofanya hivyo tambi zitakuwa na mafuta sana) Baada ya hapo zirudishe jikoni na kisha utie hiliki, chumvi, sukari, tui la nazi na maji kiasi. Zifunike kisha ziache zichemke mpaka maji yakauke. Baada ya hapo zigeuze na uzipike mpaka ziive. Nahapo zitakuwa tayari kwa kuliwa.
Updated at: 2024-05-25 10:37:48 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Bilinganya 2 za wastani Nyanya kubwa 1 Kitunguu maji 1 kikubwa Swaum 1/2 kijiko cha chai Limao 1/4 Pilipili ya unga 1/2 kijiko cha chai Parpika 1/4 kijiko cha chai Pilipili mtama 1/4 kijiko cha chai Curry powder1/4 kijiko cha chai Chumvi kiasi Coriander Olive oil
Matayarisho
Katakata bilinganya slice nyembamba kisha ziweke pembeni. Baada ya hapo kaanga kitunguu maji mpaka kiwe cha brown kisha tia swaum na spice zote, zikaange kidogo kisha tia nyanya na chumvi kiasi. Pika nyanya mpaka iive na itengane na mafuta. Baada ya hapo tia mabilinganya na ukamulie limao kisha punguza moto na uyafunike na mfuniko usioruhusu kutoa mvuke ili yaivie na huo mvuke. Baada ya hapo yaonje kama yameiva na malizia kwa kutia fresh coriander na baada ya hapo yatakuwa tayari kwa kuliwa. kwa kawaida mi hupendaga kuyalia na wali na maharage badala ya kachumari kwahiyo nakuwa naitumia hiyo kama kachumbari
Jinsi ya kuandaa Ndizi Mbichi Za Supu Ya Nyama Ng’ombe
Updated at: 2024-05-25 10:37:39 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Mahitaji
Ndizi mbichi - Kisia
Nyama ng’ombe - ½ kilo
Pilipili ya kusaga - 1 kijiko cha chai
Tangawizi ya kusaga - 2 vijiko vya supu
Thomu (garlic/saumu) - 1 kijiko cha supu
Bizari mchuzi - 1 kijiko cha chai
Nazi ya unga (ukipenda kuongezea) - 2 vijiko cha supu
Chumvi - Kiasi
Ndimu - 1 kamua
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Weka nyama ng’ombe katika sufuria, tia tangawizi, thomu, pilipili mbichi, bizari, chumvi. Roweka kidogo ukipenda kisha ikaushe yenyewe kwa maji yake Ongezea maji ya kiasi yasizidi mno, kisha funika na chemsha. Menya ndizi, ukatekate. Nyama ikikaribia kuiva, weka ndizi uendelee kupika mpaka viive vyote. Tia nazi ya unga kidogo tu ukipenda. Koleza kwa bizari mchuzi, pilipili, na ndimu Epua mimina katika chombo cha kupakulia zikiwa tayari.
Updated at: 2024-05-25 10:37:56 (1 year ago by SW - Melkisedeck Shine)
Nini maana ya lishe?
• Lishe yahusu mafunzo ya chakula na jinsi miili yetu inavyotumia chakula kamakichocheo cha ukuaji, kuzaana na utunzaji wa afya. • Lishe inajumuisha mchakato wa utoaji virutubishi vinavyohitajika kwa afya, ukuaji, kuendelea na kuishi.
Umuhimu wa lishe bora
Lishe bora ni muhimu katika mambo yafuatayo
• Utoaji nishati ili kuishi, uwepo wa mwendo, utendaji kazi, na joto. • Ukuaji, uendeleaji, ujengaji mwli, urejeshaji na utengenezaji wa seli na mikusanyika ya seli hizo (tishu) • Ufanyaji michakato ya kikemia kama vile uyeyushaji chakula, umetaboli na utunzaji mwili. • Kinga dhidi ya magonjwa, upigaji vita maambukizi na uponaji magonjwa. • Ili afya njema iweze kudumishwa, mlo wa kila siku lazima ukamilishe shughuli nne zilizotajwa hapo awali. Vyakula vinavyokamilisha moja au zaidi ya shughuli tatu huitwa virutubishi.
Virutubishi
Aina za irutubishi vikuu tunavyohitaji kwa wingi. Hivi ni:
• kabohaidreti (vyakula vya wanga, sukari na vyakula vya ufumwele): • mafuta yatokanayo na wanyama - haya yapo ya aina kadhaa • Protini- kuna mamia ya aina mbalimbali za protini. • Maji.
Virutubishi vidogovidogo tunavyohitaji kwa kiwango kidogo. Kuna aina nyingi ya hivi bali vile vinavyoelekea kukosekana kwenye mlo ni:
• madini – madini ya chuma (angalia Kisanduku cha 6, ukurasa 16), madini ya joto na zinki. • vitamnini – vitamini A, vitamini za kundi B (ikiwemo folate) na vitamini C. Kama chakula chaweza kuwa chanzo bora cha kirutubishi au la hutegemea: • Kiwango cha kirutubishi katika chakula. Vyakula vyenye viwango vingi vya virutubishi vidogovidogo kulinganisha na viwango vyake vya nguvu huitwa vyakula ‘vilivyosheheni virutubishi’ (nutrient-rich) au wakati mwingine huitwa vyakula vyenye ‘ujanzo mwingi’ wa virutubishi (nutrient dense). Vyakula hivi hupendwa kwa kuwa hutoa virutubishi vyote vinavyohitajika. Kiambatisho hiki kinaorodhesha vyakula vinavyotoa viwango muhimu vya virutubishi mbalimbali. • Kiwango cha chakula kinachotumika mara kwa mara.